loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Bil.2/- kutumika kurejesha mabalozi

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Kidawa Hamid Saleh (CCM).

Mbunge huyo alihoji kama serikali haioni kwamba kushindwa kuwarudisha watumishi waliostaafu katika Balozi zetu za nchi za nje kwa wakati stahiki, kunaiingizia gharama kubwa serikali kwa vile inaendelea kuwalipa watu hao.

Pia, alitaka kujua kama serikali haioni kwamba kitendo hicho kinavuruga mipango ya maisha ya Watanzania hao. Akijibu swali hilo, Maalim alisema fedha hizo pia zitatumika kwa ajili ya kuwapeleka watumishi wengine kwa ajili ya kuziba nafasi zilizoachwa wazi.

“Serikalii inaendelea na jitihada za kuwarejesha watumishi waliomaliza kipindi chao cha kufanya kazi Balozini na wale waliostaafu ili kutowavurugia mipango yao ya maisha,” alisema.

Alisema mwaka 2013/2014, Wizara iliwarejesha watumishi sita waliostaafu wakiwa ubalozini na kupeleka watumishi 23 kuziba nafasi zilizoachwa wazi kwenye Balozi za Beijing, Berlin, Washington, Geneva, Comoro, Kinshasa, The Hague, Kuala Lumpar, Moscow, Stockholm, Abu Dhabi, London, Dubai na New York.

Aidha, alikiri wizara hiyo kukabiliwa na changamoto ya kutowarejesha kwa wakati Mabalozi na Maofisa waliomaliza kipindi chao cha kufanya kazi balozini na wale waliostaafu.

Alisema sababu kubwa inayofanya wizara kutowarejesha watumishi hao kwa wakati ni ufinyu wa fedha za bajeti zinazotengwa katika wizara.

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi