loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bilioni 100/- kuinua ubora wa elimu

Mratibu wa Taifa wa mpango huo, Carton Aslett alisema kuwa mpango huo wa miaka minne unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ambapo halmashauri za wilaya zitakuwa mtekelezaji mkuu wa mpango huo.

Akizungumza katika warsha ya siku mbili ya utambulisho wa mradi huo kwa wakuu wa idara za elimu katika halmashauri saba za Mkoa wa Kigoma, Mratibu huyo alisema kuwa katika utekelezaji wake mpango huo utajikita katika kuangalia mafunzo ya utendaji kazi wa walimu.

Alisema maeneo mengine yatakuwa ni ya uongozi wa shule, mipango na usimamizi wa elimu ngazi ya wilaya na mkoa, ushirikishwaji wa jamii na ukusanyaji wa taarifa, takwimu na uwajibikaji.

Kwa upande wake Naibu Mratibu wa Taifa wa mpango wa Equip, James Sangoro alisema kuwa dhamira kubwa ya mpango huo ni kuwajengea uwezo walimu na wasimamizi wa elimu katika kufanya kazi yao hasa suala la ufundishaji na taaluma kwa jumla.

Sambamba na hilo alisema kuwa katika kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi mradi huo unatarajia kutoa elimu na uelewa kwa pande zote kwa maana ya walimu, wasimamizi wa elimu na jamii kuona umuhimu wa kushiriki katika shughuli na mipango mbalimbali ya kuendeleza elimu.

Akifungua warsha hiyo Mkuu wa Mkoa Kigoma, Issa Machibya alisema kuwa kutekelezwa kwa mpango huo kutakuwa chachu kubwa katika kufikia kwa haraka utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa hasa kwa mkoa huo ambao umekuwa na changamoto nyingi katika Sekta ya Elimu.

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndunguru alisema kuwa kutekelezwa kwa mpango huo iwe kichocheo kwa wadau wa elimu mkoani humo kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha mkoa unafanya vizuri kwenye Sekta ya Elimu.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi