loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bitchuka,Bella, Diamond kutengeneza wimbo

Ofisa Uhusiano wa Siku ya Msanii, Petter Mwendapole alisema jana kuwa wanamuziki ambao wameungana pamoja kutengeneza wimbo huo ni wakongwe, Hassan Rehani Bitchuka, Shakila Said, Nassib Abdul ‘Diamond’ na Christian Bella.

“Tuna wanamuziki wengi ambao wameungana pamoja katika kusherehekea siku hii muhimu kwao, kati yao wapo Hassan Bitchuka, Shakila, Christian Bella, Abdul Salvador ‘Father Kidevu’, Richard Mangustino pamoja na Mhina Panduka,” alisema.

Mwendapole alisema pia yupo Irene Sanga, Tinner Malego, Ian Mwasunga, Yohana Luhanzo, Kilimatuinde Suleiman na Ahmed Ahmed.

Alisema wimbo huo unatarajiwa kuachiwa rasmi wiki ijayo kwenye vituo vya redio na video yake itafanywa na kampuni ya Haak Neel Production lakini tayari vipande vya wimbo huo vimeanza kuonekana YouTube.

“Lengo letu ni kuhakikisha wasanii na wananchi wote wanaelewa nini maana ya sanaa, na kwamba hii ni kazi kama zilivyo kazi zingine duniani”.

MKOA wa Pwani umeanza kwa kishindo maandalizi ya kushiriki mashindano ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi