loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bodaboda wadaiwa kuua watu wawili

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Diwani Athuman alimtaja fundi uashi aliyeuawa kuwa ni Angalwisye Wilson(51) mkazi wa Mtakuja Mbalizi wilayani Mbeya.

Mwenzake waliyeuawa pamoja, hajafahamika lakini ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30-35. Alisema tukio hilo ni la Novemba 5, mwaka huu saa 1:55 asubuhi katika eneo la mlima Reli Mbalizi wilayani Mbeya.

Ilidaiwa madereva wa boda boda, walikuwa wakimtuhumu mwanaume ambaye hakufahamika jina kuiba pikipiki, yenye namba T 477 CLP aina ya CEKON.

Pikipiki hiyo inadaiwa awali iliripotiwa kuibwa katika kijiji cha Igurusi wilayani Mbarali. Ilikuwa mali ya Issa Michael (56), mkulima na mkazi wa kijiji hicho.

Kamanda alisema baada ya madereva hao kumtuhumu mwanaume ambaye hakufahamika jina, walianza kumpiga kwa kutumia fimbo, mawe na vipande vya matofali na kisha kumchoma moto.

Kwa mujibu wa kamanda, kilichomponza fundi uashi katika sakata hilo ni kuwazuia madereva hao wasiendelee kumpiga mtuhumiwa.

Ndipo walipomgeuzia kibao na kuanza kumpiga, kabla hajaokolewa na wasamaria wema na kukimbizwa katika hospitali ya teule ya Ifisi, alikofariki dunia wakati akiendelea kupata matibabu.

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema hakuna mtu anayeshikiliwa, kutokana na mauaji hayo. Polisi inaendelea kufuatilia kubaini waliohusika katika kujichukulia sheria mkononi ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.

MFUKO wa Maendeleo wa Tasnia ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo, Mbeya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi