loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bodi ya Mikopo Serikali za Mitaa kuanzisha benki

Pamoja na mambo mengine, jukumu la Msingi litakuwa ni kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwenye Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi inayolenga kuchochea uchumi.

Hayo yalielezwa leo na Mjumbe wa bodi hiyo George Lubeleje alipozungumza na Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Kibaha mjini hapa.

Lubeleje alisema kuwa Bodi ya Mikopo kwa hivi sasa imeongezewa jukumu la kutoa dhamana kwa Serikali za Mitaa ili ziweze kupata Mikopo kwenye benki ziweze kujenga na kukarabati miundombinu na kutoa huduma za msingi kwa kuchochea shughuli za kiuchumi.

Akizungumzia masharti na vigezo vya Halmashauri kupata mkopo, Lubeleje alisema sharti la msingi ni kutoa mchango wake wa akiba.

Aidha, alisema Bodi imeweka masharti na vigezo vinavyotakiwa vitimizwe ambavyo ni Baraza la Madiwani kukaa kikao rasmi na kuazimia kukopa.

Masharti mengine ni kuwepo na uthibitisho wa usimamizi mzuri wa fedha za mapato na matumizi kwa kuwasilisha hesabu zilizokaguliwa, kuwasilisha andiko la mradi linaloonesha manufaa ya kiuchumi na kijamii yatakayopatikana baada ya kuanzishwa.

Akizungumzia miradi iliyokwisha tekelezwa kwa fedha za mikopo toka Bodi hiyo, Mhasibu wa Bodi Mourice Kopalogira alisema mpaka sasa wametoa mikopo kwenye baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya ujenzi wa masoko, vituo vya mabasi, kumbi za mikutano, kilimo cha mazao ya tumbaku na zabibu.

Akihitimisha mkutano huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Addhu Dadi Mkomambo alisema umefika wakati kwa Halmashauri kutekeleza miradi yote ya maendeleo kwa kuwa sehemu ya kukopa tena kwa riba nafuu imepatikana.

“Huu ni ukombozi kwetu,” alisema.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi