loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bodi ya Mikopo ya wanafunzi kazeni buti

Mkurugenzi Msaidizi Uwezeshaji wa Bodi hiyo, Robert Kibona alibainisha hayo hivi karibuni katika mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma.

Alisema kwamba tayari waajiri watano, wameshachukuliwa hatua kwa kushidwa kutimiza wajibu huo huku wengine 18 kesi zao ziko mahakamani.

Adhabu kwa wanaopatikana na hatia kwa kosa hilo ni pamoja na kulipa faini ya Sh milioni saba ;au kutumikia kifungo kisichopungua miezi 12; au adhabu zote mbili kwa pamoja.

Tunapenda kuupongeza uongozi wa bodi hiyo, kwa kuwa na mwelekeo sahihi wa uendeshaji wa bodi yao, kwa kuanza kuhakikisha kwamba wale walionufaika na mikopo hiyo wanalipa ili kufungua nafasi zaidi kwa vijana wetu, waweze kunufaika na mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa.

Hakuna ubishi kwamba sekta ya elimu hapa nchini, inakua kwa kasi ya aina yake kutoka elimu ya awali, msingi, sekondari, sekondari ya juu na vyuo vikuu.

Tunafahamu pia kwamba vyuo vikuu tu hivi sasa hapa nchini, viko zaidi ya 19 na vingine bado vipo mbioni kufunguliwa. Kila mwaka yanapotangazwa matokeo ya mitihani ya kidato cha sita, bodi hiyo hupokea maombi ya wanafunzi lukuki ili kupata ufadhili katika masomo kwenye nyanja mbalimbali za mafunzo, wanazotaka kujiunga nazo vyuo vikuu.

Sote ni mashahidi kwamba kila mwaka mamia kwa maelfu ya vijana wetu wa kike na kiume, hukosa kupata ufadhili kwa sababu mbalimbali, ikiwemo ukweli kwamba fedha zinazotengwa na Bodi kwa ajili ya udhamini wa wanafunzi, hazitoshi.

Kama hali ndiyo hiyo na wote tunaijua, huku pia kwa upande mwingine waajiri ambao ndiyo wanaofurahia huduma inayotolewa na vijana wetu tena baada ya kufadhiliwa na Bodi, kwa nini wasione umuhimu wa kuhakikisha kwamba wanaisaidia bodi hiyo, kutekeleza majukumu yake kwa kuwapatia taarifa hizo muhimu ili wahusika wabanwe kulipa mikopo hiyo?

Ukakasi huu unatoka wapi na unafanywa kwa faida ya nani? Hivi ukitoa taarifa wewe kama mwajiri, unapoteza nini, zaidi ya kusaidia maelfu ya vijana wetu wanaokosa elimu kwa sababu ya uwepo wa fedha ndogo zilizotengwa kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi?

Hatua hii ya Bodi ya Mikopo, inatakiwa kuungwa mkono na kila Mtanzania, anayependa elimu ili sote kwa pamoja tuweze kuliendeleza taifa, lenye uwezo na upeo wa juu katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni.

Utanufaika nini kwa kufikishwa mahakamani na kisha kutwikwa adhabu hizi zilizotajwa? Tafadhali kwa wale waajiri ambao wamejisahau, wakumbuke sasa kutimiza wajibu wao kabla hawajafikwa na mkono wa sheria. Tuwape ushirikiano wenzetu hawa.

UCHAGUZI Mkuu wa madiwani, wabunge, wawakilishi, Rais wa Zanzibar na ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi