loader
Picha

Bonanza la ufukweni kufanyika leo

Bonanza hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa kamati ya mchezo huo na wadau chini ya udhamini wa Taasisi ya Mwangaza wa Burudani Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kiongozi wa bonanza hilo, Muslim Nassor alisema bonanza hilo litaongozwa na waamuzi waliopata mafunzo maalumu ya mpira huo na elimu iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

Nassor alisema kwa mantiki hiyo, bonanza hilo litafuata vigezo na masharti ya Fifa na linatarajiwa kuanza saa nne asubuhi kwa burudani asili na mchezo mbalimbali. Alifahamisha timu nane zitashiriki bonanza hilo ambalo linatarajiwa kujumuisha wageni wasiopungua 400.

Timu zitashiriki bonanza hilo ni ZIFF, Kendwa Rocks Hotel, Clove Hotel &Shisha Lounge, Comnet Connaction, Makontena, ZABECO Centre, Nungwi na Galaxy.

MABINGWA wa kihistoria Yanga leo wanashuka dimbani kuikabili Tanzania Prisons ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi