loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bongo Movies washindwa kutumia fursa ZIFF

Tamasha hilo lililofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi katika ukumbi wa Ngome Kongwe Visiwani Zanzibar, limekosa ushiriki kamili wa Bongo Movies ambao kelele zao kubwa ni soko na kujijenga kimtandao.

Katika mikutano mingi ya waandishi wa habari waigizaji waliokuja kama Terry Pheto wa Afrika Kusini, mtengeneza sinema Umar Turaki kutoka Nigeria wamekuwa wakitafuta watu wa kufanya nao shughuli nchini Tanzania bila mafanikio.

Wasanii wa Bongo Movie ambao walionekana katika viunga vya maeneo ya sinema ni Irene Sanga, Ali Yakuti na Nasri ambao ni miongoni mwa watu 15 walioshiriki katika programu ya Maisha Lab ambapo Nasri aliibuka mshindi.

Kutokuwepo kwa wasanii wa Bongo Movie na hata balozi wao ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Saimon Mwakifamba kunaleta hisia isiyo sahihi kwa wahakiki wa sinema ambao wamekuwa wakishauri Watanzania kulitumia tamasha la ZIFF kujifunza na kutanua mtandao wa maelewano na wasisubiri kualikwa.

“Wapo watengeneza sinema wengi wanakuja bila kualikwa, nia ni kukuza mtandao wa mawasiliano na kuona fursa za soko” anasema Meneja wa Tamasha Daniel Nyalusi wakati alipokuwa akijibu swali la mwaliko.

Alisema tamasha ni la kila mmoja lakini wapo watu wanatoka Haiti wanakuja kwa fedha zao na kuja kuona fursa ya soko na kusikia wengine wanafanyaje kazi zao.

Wasanii na watengeneza sinema wa Kenya, wamejitokeza kwa wingi na kazi zao wakitumia ZIFF kama sehemu ya kujitangaza.

Akizungumzia kuhusiana na wasanii wa filamu nchini kutokuwepo katika uzinduzi wa tamasha na hadi juzi, Mkurugenzi wa Ziff, Profesa Martin Mhando alisema wasanii hao hawaoni umuhimu wa tamasha.

“Tatizo kubwa hapa ni kwa wasanii wetu wengi wao wanasubiri sisi waandaaji tuwaombe waje kushiriki katika tamasha hili baada ya wao waje kuomba ama kuja kujifunza binafsi katika tamasha hili,’’ alisema.

“Nawalaumu kwa kuwa hawalichukulii tamasha hili kwa uzito,” alisema Profesa Mhando na kuongeza kuwa kama wangekuwepo labda wangeweza kupata elimu na kubadilishana mawazo na magwiji mbalimbali waliofika.

Hata hivyo Mhando alisema wasanii wa Bongo Movie watafika kesho kama walivyoombwa na uongozi wa Ziff kwa ajili ya siku ya Swahili Day.

Kuna sinema kadhaa zilizoingia katika ushindani wa tamasha ingawa ipo siku kamili ya kuonesha sinema za Kiswahili na ushindani katika awamu hiyo hiyo.

KOCHA wa timu ya taifa, ‘Taifa ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi