loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bongo Star Search yanoga, Kahoza nje

Pia katika shindano hilo linalodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel na kuoneshwa na luninga ya TBC1, mshiriki Godfrey Kahoza aliyaaga mashindano hayo.

Kundi la kwanza lilikuwa ni la timu ya Salama Jabir ambalo lilikuwa na waimbaji kama vile Melisa John ambaye namba yake ya kupigiwa kura ni 22 na Joshua Kahoza ambaye namba yake ni 02.

Melisa huku akiwa amevalishwa na City Star Boutique, alianza kwa kuimba wimbo msanii wa Marekani, Rihanna uitwao Stay aliouimba vizuri.

Alifuata mshiriki Joshua Kahoza ambaye aliimba wimbo wa Mapenzi gani wa Banana Zorro. Baada ya kumaliza kuimba, ilifuata timu ya Jaji Master Jay ambayo ilikuwa na washiriki kama vile Amina Chibaba ambaye namba yake ya ushiriki ni 03 na Emmanuel Msuya ambaye namba yake ya ushiriki ni 21.

Amina aliimba wimbo wa Nataka Niwe Wako wa Maunda Zoro, wakati Msuya aliimba wimbo wa Aifola wa Linex ambapo tofauti na ilivyozoeleka, huwa anaimba kwa kutumia gitaa, lakini jana aliimba kwa kinanda.

Ikafika zamu ya washiriki wa Jaji Ritha Paulsen ambao walikuwa ni Maina Thadei mwenye namba ya ushiriki 15, Mandela Nicolaus namba 10 na pia Elizabeth Mwakijambile ambaye namba yake ya ushiriki ni 08.

Maina alianza kwa kuimba wimbo wa taarabu wa Ewe Njiwa wa Patricia Hillary akifuatiwa na Mandela Nicolus aliyeimba wimbo wa Jamila wa Chameleon.

Uimbaji wa jana ukamalizika kwa kuimba Elizabeth aliyeimba wimbo wa Mkono Wako wa Efraim Sekereti ambapo naye aliuimba kwa umakini.

Wakati huo huo, washindi wa shindano la kupiga kura wametangazwa wiki hii, ambapo Irene Shirima alishinda simu ya mkononi kutoka Samsung, na Shadat Suleiman ambaye ameshinda modemu ya Zantel.

Washindi wengine ni Jane Augustino, Salma Mohamed, Tausi Swalehe, Hussein Ramadhan, Maureen Mwaiko, Maria Ipono, Maximillian Lupapa, Maimuna Tabu na Ramadhan Yusuph.

Ritha akizungumza na gazeti hili aliwataka watu waendelee kuwapigia kura washiriki huku akisisitiza kuwa wanatakiwa kuandika namba za ushiriki za washiriki husika na kisha kutuma kwenda 15530.

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: DAILY NEWS Reporter

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi