loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

BoT yalinda amana za wateja FBME

Kwa sasa Msimamizi wa Masuala ya Benki wa BoT, Lawrence Mafuru, ndiye msimamizi wa benki hiyo, ambaye katika mazungumzo maalumu kwa njia ya simu jana, aliwatoa hofu wateja wa benki hiyo kuhusu usalama wa amana zao na biashara za benki hiyo hapa nchini.

"Chini ya uangalizi wa Benki Kuu, nimeteuliwa kulinda amana za wateja wa FBME na kuhakikisha kazi za kila siku za benki hiyo zinaendelea kama kawaida,” alisema Mafuru. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Taasisi ya Kushughulikia Uhalifu Katika Masuala ya Fedha (FinCEN) iliyo chini ya Hazina ya Marekani, kudai FBME kuwa taasisi ya fedha inayojihusisha na utakatishaji fedha.

“Marekani haiwezi kuruhusu taasisi yoyote ya kifedha kutuma fedha chafu nchini kupitia mfumo wetu wa fedha,” alidai Mkurugenzi wa FinCEN, Jennifer Calvery. Taasisi hiyo imeituhumu FBME kwa kupuuza mikakati ya kuzuia utakatishaji wa fedha na kujikuta ikitumika kwa vitendo viovu.

Tuhuma hizo zilipotolewa kwa mara ya kwanza mwaka jana, benki hiyo ilikanusha na kudai kuwa wakaguzi wa mahesabu, wamethibitisha kuwa imekuwa ikifuata taratibu za kukabiliana na utakatishaji fedha, zinazosimamiwa na Benki Kuu ya Cyprus na Umoja wa Ulaya (EU).

Pamoja na kukanusha huko, Benki Kuu ya Cyprus mwaka huo huo, iliamua kusimamia uendeshaji wa benki hiyo baada ya taarifa hiyo ya FinCEN.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imempandisha kizimbani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi