loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘CCM imara bila Lowassa’

Kimesema kitashinda uchaguzi huo kwa sababu kinajivunia utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi na uteuzi makini wa mgombea wao wa urais, Dk John Magufuli aliyeteuliwa kwa asilimia 87 ya kura za wajumbe wa Mkutano Mkuu.

Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Lowassa aliingia katika CCM kwa ridhaa yake bila kushurutishwa, hivyo ana haki ya kuhamia chama kingine.

“Lowassa aliingia CCM kwa ridhaa yake bila kushurutishwa, aliipenda CCM na kwa ridhaa yake ameamua kuingia chama kingine. CCM itabaki kuwa imara na itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba,” alisema Simba.

Alisema CCM inaamini kuwa chama kwanza mtu baadaye, na kwamba mfumo wa kuondoka ndani ya chama hicho hakuanza kwa Waziri Mkuu huyo wa zamani, bali kwa wanasiasa wengine kadhaa akiwataja Mwenyekiti wa sasa wa TLP, Augustine Mrema na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

“Mfumo wa kuondoka CCM haukuanza na Lowassa, wapo wengi waliondoka kwa ridhaa yao. Yupo mtu hapa alitoka na gari lake kusukumwa nchi nzima…anaitwa Mrema. Slaa alikuwa CCM, Mrema alikuwa very strong (madhubuti). Lakini CCM itashinda, tena asubuhi,” alitamba Katibu huyo.

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Lowassa aliihama CCM juzi na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiandaliwa kuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NLD na NCCR-Mageuzi.

Lowassa alisema anaondoka CCM kwa sababu hakutendewa haki katika mchakato uliomuibua Dk Magufuli kuwa mgombea urais wa chama tawala, akidai kuwa uligubikwa na mizengwe, ukiukwaji wa maadili, uvunjaji wa Katiba na taratibu za uchaguzi za CCM, na dhahiri, uchaguzi ulisimamiwa kwa upendeleo na chuki dhidi yake.

Lakini Simba alisema chama hicho kitashinda ‘asubuhi’ kwa sababu kimetekeleza kwa ukamilifu Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kimeteua mgombea anayekubalika na umma na anauzika. “Tutashinda asubuhi, hatuna wasiwasi.

Tutashinda kwa kura za haki kwa sababu tuna mgombea anayekubalika na kuuzika. Mtusubiri katika majukwaa ndio mtajua tunashindaje,” alisema Simba maarufu Gaddafi.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mgaya Kingoba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi