loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

CCM yamuenzi Nyerere kwa kuzindua matawi

Akizindua mashina hayo jana, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba `Gaddafi’ alisema katika kumuenzi Baba wa Taifa wameamua kufanya kazi za chama kuhakikishakinaendelea kudumisha amani ya nchi.

Mashina yaliyozinduliwa ni la wakereketwa la madereva teksi wa Feri Sokoni, wa Kanisani na shina la wakereketwa wa Midizini.

“Uzinduzi wa mashina haya ni chachu ya kuongeza wanachama wa CCM na kuweka kikosi kazi cha CCM katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kuhakikisha Dar es Salaam inaendelea kuwa ngome ya CCM,” alisema.

Alisema mtaji wa siasa ni kutafuta wanachama, hivyo watahakikisha wanajenga kikosi imara kitakachosaidia kurudisha kata zote na majimbo yaliyopotea sanjari na kusimamia Katiba ya nchi.

Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa alisema watahakikisha wanaongeza idadi ya wanaCCM sanjari na kuhakikisha Ilani ya chama hicho inatekelezwa kikamilifu.

foto
Mwandishi: Hellen Mlacky

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi