loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Changudoa Dodoma eti nao wasomi wa vyuo!

Inakadiriwa kuwa yawezekana wanafunzi zaidi ya 15,000 wako katika vyuo vya elimu ya juu vilivyoko hapa mji huu mkuu wa bongo.

Kuna cha Mtakatifu John, UDOM ambacho kinabeba hadhi ya kimataifa, CBE, mipango na vyuo vingine kama kile cha serikali za mitaa kilichoko Hombolo. Haya yote ni mavyuo yenye wanafunzi lukuki. Watu wa Dodoma wakafurahi kwamba mkoa wao sasa ni kitovu cha elimu.

Lakini maendeleo nayo yanakuja na yake, bei ya bidhaa nayo imepanda ajabu. Pande la mbuzi ambalo awali ulinunua kwa Sh 1,500 leo hii utaambiwa ni Sh 3,000 bei ambayo ni sawa tu na ile ya Nderingo, Deluxe na baa zingine nyingi tu.

Hata walaji wa kiti moto nao hawana nafuu, Sh 2,500 ndio bei ya awali hali ambayo inawafanya wajione tu kama wako katika jiji la Lukuvi.

Hivyo maendeleo tuliyolilia Dodoma yamekuwa laana, vitu vimepanda bei, kwenye mabenki foleni nazo haziishi. Kilichosalia ni foleni tu ya magari ambayo nadhani pia baada ya miaka mitatu itakuwa kama Dar.

Hata vyumba vya kupanga navyo bei ziko juu, kwa wale ambao hatuna makazi ya kudumu tulizoea kulipa Sh 10,000 au Sh 12,000, lakini leo hii bei ya chini ni Sh 15,000 katika gesti nyingi.

Hiyo ndio Dodoma kwamba maendeleo yamekuwa balaa. Ombaomba badala ya kulima kwa vile kuna mashamba mengi, wao nao hawataki kutegemea kilimo cha huruma ya Mungu, wameendelea kupita kila baa kuomba wasaidiwe.

Wakija Dar wanaomba, wakiwa hapa Dodoma pia wanaomba, usishangae unataka akalime wakati kilimo hakina tija! Basi ni balaa tupu katika mji wa Dodoma. Juzi mtu mmoja kaninong’oneza ukitaka kiwanja maeneo ya mjini ni balaa bei yake kama ile ya Segerea.

Lakini kwa wale wanaoishi sasa mji mpya, imekuwa kama Kariakoo ambako watu wananunua nyumba wanajenga magesti.

Huu ndio uwekezaji wa watu wa Dodoma na hawafikirii kujenga hoteli kama ilivyo Kariakoo. Baada ya miaka mitano, yawezekana mji mpya ukawa umejaa gesti tu! kwani hakuna uwekezaji wanaojua ndugu zangu Wagogo zaidi ya huu wa kujenga gesti.

Si wanajua kila baada ya miezi miwili Bunge linakaa, maofisa wa serikali kwa uroho wa fedha za umma hata kama wizara yake ina siku moja ya kuwasilisha bajeti lazima atakuja kukaa wiki moja.

Acha bajeti, unaambiwa hata kama wizara yake ina swali moja la kujibu kwa wiki, afisa lazima achukue masurufu ya wiki moja. Kisa ni kwa ajili ya swali moja tu.

Kwa nini Wagogo wasijenge utitiri wa gesti? Mambo ya Dodoma mengi ndugu yangu, nikiyataja siwezi kuyamaliza. Cha ajabu hata Changudoa nao ambao wanamiminika kutoka mikoani wakati wa Bunge nao wamebuni mtindo mpya wa kuwanasa waheshimiwa.

Wameshajua baadhi ya waheshimiwa ni wagonjwa wa totozi wa vyuoni, wanajua watoto wa vyuo ndio wenye soko.

Nao wamebuni mtindo wa kubeba madaftari kwenye mikoba yao ya mkononi. Muulize habari zako na unafanya wapi kazi? Atakwambia nasoma Mipango, CBE au UDOM.

Wanazijua hata kozi zinazoendeshwa kwenye vyuo hivyo kumbe hakuna lolote ni ma-CD wako kwa ajili ya biashara ya kunasa mahela lukuki ya baadhi ya waheshimiwa na maofisa wa serikali. Si wanajua wanafunzi wengi wanakaa off-campus, kwa hiyo kwa CD kusema anakaa nje ya chuo sio jambo la ajabu. Kwa hali hiyo nao wameshawanasa wengi tu.

Mtu anabeba changudoa anadhani kabeba mwanafunzi wa UDOM. Kumbe wapi, wameshaingia mkenge.

Walitaka kuwatosa ma CD nao wakabuni mbinu za kuendelea kuwanasa. Hayo ndiyo mambo ya DOM kwa wale mnakuja hapa kuweni makini msije mkaingia mkenge kama huu wanaoingia wengine.

Kama una maoni tuwasiliane. 0767 341 418.

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Shadrack Sagati

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi