loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

China, Tanzania zaandaa maonesho

Mwakilishi wa uchumi na Biashara wa China nchini, Wang Fang alisema maonesho hayo yatakayofanyika ukumbi wa Diamond Jublee yatashirikisha kampuni zaidi ya 100 kutoka mikoa na manispaa 12 nchini China.

Alisema maonesho hayo yatagawanywa katika sehemu nne kutokana na aina ya bidhaa za viwandani ambazo ni biadhaa za mashine na magari, vyombo vya umeme vya majumbani.

Fang alisema makundi mengine ni bidhaa za walaji na vifaa vya ujenzi, kemikali, matibabu na yenye matumizi zaidi ya moja.

“ Tunaamini kwamba maonesho ya bidhaa za China Afrika itakuwa mojawapo ya jukwaa muhimu ya mawasiliano ya biashara na ushirikiano kati ya China na Afrika, ambalo itasaidia kufikisha faida za pande mbili.

Fang alisema maonesho hayo pia ni njia ya kukuza maendeleo mapya ya ushirikiano wa mtindo mpya wa kimkakati kati ya China na Tanzania. Maonesho hayo ni ya tatu kufanyika nchini.

Kwa mara ya kwanza maonesho hayo ya kila mwaka yalifanyika mwaka juzi.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi