loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

China yaipa TAZARA magari 100

Misaada hiyo ilikabidhiwa Dar es Salaam jana na Makamu wa Rais wa China aliyeko nchini kwa ziara ya kikazi Li Yuanchao kwa niaba ya Serikali yake kwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa magari hayo 10, Dk Mwakyembe, alisema misaada hiyo ni sehemu ya misaada inayotolewa kila mwaka kwa shirika hilo na China, lengo likiwa ni kuimarisha utendaji wake.

“Leo tumekabidhiwa magari haya ikiwa ni sehemu ya kwanza ya msaada kutoka China, pamoja na magari haya makubwa ya winchi manne, na Makamu wa Rais ameahidi kuongeza nguvu kifedha zaidi kuboresha shirika hili,” alisema Mwakyembe.

Alisema pamoja na kukabidhiwa misaada hiyo, pia Makamu huyo wa Rais wa China, alikagua stesheni hiyo ya Tazara akiangalia ubora wake baada ya miaka 40 tangu kuanza kufanyakazi.

“Tulikuwa tunakabiliwa na wakati mgumu katika kipindi cha utawala wa mabavu, tukaomba nchi mbalimbali msaada zikakataa lakini China pekee ilitusaidia, ikajenga reli hii ya Tazara na kuisaidia Zambia kupitisha mizigo yake,” alisisitiza.

Alisema reli hiyo ya Zambia ina urefu wa kilometa zaidi ya 1,800 ikiwa na madaraja na makalavati zaidi ya 300.

Alisema Serikali za Zambia na Tanzania zinatarajia kukutana Julai 2, mwaka huu ili kujadili namna ya kuiendeleza na kuboresha huduma za shirika hilo.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais Yuanchao alisema amefurahishwa na namna Serikali ya Tanzania na wafanyakazi wa Tazara walivyomudu kulitunza shirika hilo na mali zake pamoja na umri mkubwa wa shirika hilo, na kuahidi kuwasiliana na nchi yake ili kuona namna ya kusaidia zaidi katika kuliimarisha.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi