loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chuo cha Nyuki kupandishwa hadhi

Alisema kutokana na umuhimu wa chuo hicho, atahakikisha kinaboreshwa zaidi kiwe kitovu cha ubora katika taaluma ya sayansi ya misitu na nyuki na hifadhi zake. Alisema kwa kuanzia, atawasiliana na wataalamu wa wizara hiyo, wahuishe mitaala yake kukiongezea hadhi.

“Tunataka chuo hiki kiwe kimbilio la wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchi, tutakiboresha zaidi ili kiwe kitovu cha ubora katika sayansi ya misitu na nyuki,” alisema Nyalandu.

Aliongeza kuwa wizara yake itashughulikia changamoto zote zinazokikabili, ikiwemo upungufu wa watumishi kuhakikisha chuo hicho na sekta zingine zilizoko ndani ya wizara hiyo, zinakuwa na watumishi wa kutosha na kutoa fursa za ajira kwa askari wa wanyama pori na wataalamu wengine.

Lengo ni kuhakikisha ulinzi wa kutosha, unakuwepo katika maeneo yote ya hifadhi za misitu na kuwezesha shughuli zote katika maeneo hayo, ikiwemo ufugaji nyuki.

Awali, akisoma risala , Mkuu wa Chuo hicho, Semu Daud alisema tangu mafunzo ya chuo hicho yarudishwe rasmi mkoani Tabora , kimeanza kupata mafanikio makubwa, ikiwemo kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 34 mwaka 2010/2011 hadi 115 kwa mwaka 2014/15.

Alisema wanafunzi 58 wa kike na kiume kwa mwaka 2013/14, wamehitimu mafunzo hayo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada ya Ufugaji Nyuki.

Alitaja mafanikio mengine kuwa ni chuo kupata utambulisho maalumu wa ithibati ya muda kutoka Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) .

Alisema ili kuthibitisha umuhimu wa taaluma inayofundishwa na chuo hicho, wamepewa fursa ya kushiriki katika Maonesho ya Biashara na Kilimo (Sabasaba na Nanenane) tangu mwaka 2009 mpaka sasa kuelimisha wananchi.

RAIS John Pombe Magufuli anaongoza kwenye ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi