loader
Dstv Habarileo  Mobile
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji chaeleza mafanikio, mikakati

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji chaeleza mafanikio, mikakati

Mkuu wa chuo hicho, Mhandisi Dk Zacharia Mganilwa, anasema kwamba chuo kimepitia historia ndefu kwani kilianzishwa mwaka 1975 kama sehemu ya mafunzo ya lililokuwa Shirika la Usafirishaji la Taifa (NTC) na kilikuwa na wajibu wa kuiendeleza nguvu kazi ya sekta usafirishaji pamoja na mameneja wa kada ya kati wa NTC.

Baadhi ya mashirika yaliyokuwa chini ya NTC ni Kampuni ya Mabasi Tanzania (KAMATA), Shirika la Usafiri Dar es Salaam( UDA) na Makampuni ya Usafirishaji ya Mikoa. Mwaka 1982, Chuo kiliboreshwa zaidi na kutoa mafunzo katika nyanja mbalimbali za usafirishaji, na kikawa chini ya Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano na kikaanza kazi mwaka 1983 chini ya maboresho hayo.

Kwa sasa chuo kiko chini ya Wizara ya Uchukuzi na kimesajiliwa na NACTE. Katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya uongozi wa Dk Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mambo mengine Chuo kimefanya mambo mengi sana kama anavyoeleza Mkuu huyo wa Chuo.

Dk Mganilwa anasema kwamba alipojiunga na chuo hicho mwaka 2011 kwa kushirikiana na uongozi mzima wa chuo, serikali, walianzisha mageuzi makubwa yenye lengo la kukiboresha chuo ili kufundisha masomo yanayokidhi mahitaji ya soko.

“Niliamua kuweka mkakati wa miaka mitano ambao kwa kushirikiana na wenzangu tuliamua kuutekeleza kwa nguvu moja ili chuo chetu kiwe kitovu cha ubora hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla,” anasema. Anasema katika kufanikisha mageuzi hayo, ilibainika kwamba ni muhimu kubadilisha majina ya idara zilizokuwepo ili ziweze kubeba programu nyingi zaidi kufuatana na mahitaji ya soko.

Aidha waliona pia ni muhimu kuanzisha idara mpya za taaluma ili ziweze kwenda sanjari na mageuzi hayo. Anayataja majina ya zamani ya idara na majina mapya kwenye mabano kuwa ni Logistics and Transport Management (LTM) (Logistics and Transport Studies LTS). Automobile Engineering (AE) (Transport Engineering and Technology TET).

Mengine ni Information and Communication Technology and Learning Resources ICT (Computing and Communication Technology (CCT), General Studies GS (Mathematics, Humanities and Social Sciences, MHSS), Road Safety RS, ( Transport Safety and Environmental Studies TSES) na Research, Consultancy and Publication (RCP) (Research, Publications and Post Graduate Studies (RPGS).

Majina mengine ni Library Services (LS) (National Transport Resources Centre, NTRC) na Centre For Continuing Education (Centre for Profession Development CPD) na Centre for Continuing Education (CCE), (Centre for Professional Development CPD). Anasema kwamba idara nyingine nne zaidi zimeanzishwa ili kukidhi haja ya uanzishwaji wa programu nyingine ambazo yamkini haziwezi kubebwa na idara hizo nane zilizotajwa hapo juu.

Idara mpya nne zilizoanzishwa na kufanyiwa utambuzi na NACTE ni Business and Entrepreneurship Studies (BES), School of Aviation Studies (AS), Research and Postgraduate Studies (RPS),Consultancy and Production Bureau (CPB). Anasema kwamba baada ya muundo mpya wa Idara, Chuo kina jumla ya programu 27 ikiwa programu moja ni ya Shahada ya Uzamili , saba za shahada ya kwanza, tisa za Stashahada ya Uzamili na kumi za Stashahada.

Kuhusu namna chuo kilivyojipanga kutayarisha rasilimali watu watakaokidhi matakwa ya soko la ajira katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji, Dk Mganilwa, anasema kimejipanga katika sekta mbalimbali.

Usafiri wa njia ya barabara. Anasema sekta hii inakabiliwa na uwepo wa magari mabovu barabarani, ajali nyingi za barabarani, msongamano mkubwa wa magari mijini na hasa Jiji la Dar es Salaam pamoja na uchafu wa mazingira kutokana na vyombo vya moto vya usafiri.

Anasema kwamba ili wahitimu waweze kuzikabili changamoto hizo chuo kimefanya mambo kadhaa ikiwamo Mitaala ya Stashaha da na Shahada ya Uhandisi magari imehuishwa ili kutoa wahitimu waliobobea kukabiliana na changamoto hizo.

Mtaala mpya umetengenezwa kwa ngazi ya Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Usalama wa Usafiri wa Barabara (Postgraduate Diploma in Road Transport Safety Management), ambao umeanza kutumika Januari mwaka 2013.

“Hii imelenga kufundisha wataalamu waliobobea katika ngazi ya kati na ya juu yaani middle and Senior level expert katika masuala ya usalama barabarani,” anasema. Anafafanua kuwa mitaala ya kufundishia madereva wa mabasi ya abiria, magari ya mizigo, magari ya viongozi, waalimu wa madereva na wakaguzi wa magari imeboreshwa na sasa iko katika kiwango cha kimataifa.

Mkakati mwingine ni ununuzi wa seti nne za kisasa za ukaguzi wa magari ambazo zitatumika kufundishia wataalamu wa ukaguzi wa magari na ambapo kwa sasa kituo hicho cha ukaguzi kimeanza kujengwa na kiko katika kiwango cha asilimia 80 ili kiweze kukamilika na hatimaye kianze ukaguzi huo Januari 2014.

Usafiri wa Majini Huduma ya usafiri wa majini inakabiliwa na matatizo ya ufanisi mdogo wa bandari zetu katika kushughulikia mizigo na usalama wa abiria.

“Ili wahitimu wetu waweze kuzikabili changamoto hizo chuo kimefanya yafuatayo,” Mitaala ya Stashahada na Shahada katika Menejimenti ya Lojistiki na usafirishaji na upokeaji na upelekaji shehena imehuishwa ili kutoa wahitimu waliobobea kuweza kukabiliana na changamoto zilizotajwa hapo juu, hii ni kwa upande wa operational staff .”

Anasema kwamba mtaala mpya umetengenezwa kwa ngazi ya stashahada ya uzamili katika menejimenti ya usafiri wa meli na uongozi wa bandari. Anabainisha mtaala huo ulianza kutumika mwaka 2012 na kwamba umelenga kufundisha mameneja waliobobea katika ngazi ya kati na ya juu yaani middle and senior managers katika masuala ya bandari.

“Idara iliyokuwa inaitwa Road safety imebadilishwa na kuwa Transport Safety and Environmental Studies ili iweze kushughulika na usalama katika huduma ya majini pia. Usafiri wa anga Sekta hii inakua kwa kasi kwa wastani wa asilimia kumi na mbili kwa mwaka. Rasilimali watu katika sekta hii ina changamoto kubwa na nyingi.

“Mafundi na Wahandisi wa ndege waliosoma enzi za Shirika la Ndege la Afrika Mashariki ni wachache sana, wengi wamestaafu na walio kazini wanakaribia kustaafu . Kwa upande wa marubani wazawa hali si shwari pia,takwimu zinaonesha kuwa marubani wazawa wako 183, mahitaji kwa ndege zilizopo ni marubani 456 hivyo marubani waliopo nchini ni 273 sawa na asilimia 60.

Anafafanua kuwa uchache wa wahandisi na marubani wazawa unatokana na kutokuwa kwa vyuo vya mafunzo hapa nchini kwani mafunzo kwa sasa yanapatikana nje ya nchi kwa gharama kubwa ambazo wazazi hata mashirika ya ndege yenyewe hayawezi kumudu kusomesha vijana wa kutosha.

Dk Mganilwa anasema kumsomesha rubani au mhandisi mmoja ni gharama yake ni ni karibu Shilingi milioni 100, Je ni Watanzania wangapi wanaoweza kumudu? Kuhusu eneo hilo anasema NIT imefanya yafuatayo, kuanzisha Shule mpya ya Mafunzo ya Teknolojia ya Usafiri wa Anga (School of Aviation Technology), ambayo imeshafunguliwa.

“Mitaala ya stashahada na shahada katika Menejimenti ya Lojistiki na Usafirishaji imehuishwa ili kutoa wahitimu waliobobea kuweza kukabiliana na changamoto katika sekta ya anga, ambao ulianza kutumika mwaka jana, ” anafafanua. Dk Mganilwa anasema kwamba kwa kushirikiana na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wamekamilisha kutengeneza mitaala ya kufundisha mafundi wa ndege na wataalamu mbalimbali wa kuhudumia ndege hapa nchini .

“Tumeomba ithibati kutoka Mamlaka ya Usalama wa Anga (TCAA) ili tuweze kudahili wanafunzi, mipango pia inafanywa kuona namna pia tutakavyoweza kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania upande wa airwing na mazungumzo ya awali yamefanyika.” Anatoa shukrani kwa Wizara ya Uchukuzi kwa kuwapatia uwanja wa Dodoma na Tanga kwa madhumuni ya kujifunza na kwamba Mitaala imewasilishwa TCAA kuomba ithibati.

“Tunawashukuru sana Kampuni ya AERO- LEASE INVESTMENT kwa kutupatia ndege itakayotumika kwenye mafunzo ya marubani kwa ngazi ya PPL,”anasema na kuongeza kuwa kwa kushirikiana na Wakala wa Ndege wa Serikali (TGFA) wanakamilisha utaratibu wa kufundisha marubani walio na leseni za PPL kusomea mpaka ngazi ya CPL.

Usafiri kwa njia ya Reli Sekta hii kama ilivyo ya anga inakabiliwa na uhaba mkubwa wa rasilimali watu, pamoja na uchakavu wa miundombinu, Injini , mabehewa na njia zote za reli vyote vimechakaa, serikali nayo kwa upande wake imeweka mikakati ya kufufua usafiri wa reli.

Anasema katika kusaidia usafiri wa reli wanafanya yafuatayo: NIT imehuisha mitaala ya Stashahada na Shahada katika Menejimenti ya Lojistiki na Usafirishaji na Upokeaji na Upelekaji Shehena imehuishwa ili kutoa wahitimu waliobobea kuweza kuihudumia sekta hii.

Anabainisha kuwa Mitaala mipya imetengenezwa kwa ngazi ya Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti na Uendeshaji ya Usafiri ya Reli na Uchumi katika Usafirishaji (Postigraduate Diploma in Transport Economics)ambayo imeanza kutumika Januari 2013.

“Hii imelenga kufundisha mameneja wataalamu waliobobea katika ngazi ya juu yaani Middle and Senior level Managers katika masuala ya usafiri wa reli. Anasema NIT imeingia mkataba na TRL-Chuo Cha Reli Tabora na Kampasi ya Morogoro ambao mitaala ya NIT iliyo na ithibati ya NACTE inaboreshwa ili kuweza kutoa wataalamu mbalimbali sekta ya reli katika kozi zifuatazo.

Diploma in Automobile Engineering and Locomotive Technology, Diploma in Mechanical Engineering and Locomotive technology, Diploma in Mechanical Engineering and Marine Technology, Diploma in Logistics and Rail Transport Management, Diploma in Electronics, Telecommunication and Signalling Engineering na Diploma in Civil and Railway Engineering.

Anasema kutokana na uhaba wa wataalamu wazawa katika ushauri wa miradi au makandarasi wa kujenga miundombinu ya usafirishaji miundombinu ya reli na mabomba, Chuo kimeamua kufanya yafuatayo: Kutengeneza mtaala mpya wa ngazi ya Stashahada ya Uzamili katika Uhandisi Usafirishaji Postgraduate Diploma in Transportation Engineering with specialization in ,Airport Engineering, Railway Engineering, Port and Habours Engineering na Pipeline Engineering ) ambao umeanza kutumika tangu Januari 2013.

“Hii inalenga kufundisha wataalam wahandisi waliobobea katika usanifu, ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege, bandari, njia za reli, mifumo ya mabomba kwa ajili ya gesi na mafuta. Katika mwaka wa masomo wa 2013/14, katika ngazi ya Stashahada,Uzamili, Astashahada na Shahada ya kwanza, chuo kimedahili jumla ya wanafunzi 1582, ikilinganishwa na wanafunzi 945 waliodahiliwa katika mwaka wa masomo uliopita.

Anasema hilo ni ongezeko la wanafunzi 637 sawa na asilimia 67 katika ongezeko la wanafunzi wanaoendelea na masomo ni 1207. Jumla ya wanafunzi kwa sasa ni 2789. Chuo kwa sasa kinaandaa kozi mpya ambazo ni Bachelor Degree in Accounting and Transport Finance, Bachelor Degree in Economics and Transport Planning, Bachelor Degree in Transport Marketing Management na Bachelor Degree in Freight and International Trade.

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi