loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chwaka, Ngome zang’ara daraja la kwanza

Chwaka ambayo ilicheza katika uwanja wa Hanyegwa, Mchana iliifunga KVZ mabao 2-0 wakati Ngome iliifunga Kimbunga mabao 2-1.

Chwaka ilifanikiwa kushinda katika kipindi cha pili kupitia kwa wachezaji wake Mohammed Omar katika dakika ya 71 na Haruna Kassim aliyefunga dakika ya 87.

Na katika uwanja wa Tazari ambapo timu ya Kimbunga ilikuwa nyumbani, ilishindwa kuutambia uwanja wake huo na kukubali kipigo cha mabao 2-1 huku wakiwa wao ndio waliotangulia kupata bao katika dakika ya 15 kupitia kwa mchezaji wao Khamis Hija.

Wafungaji wa Ngome katika mchezo huo walikuwa Juma Pandu, dakika ya 35 na Khatibu Kaimu aliyezifumania nyavu za wapinzani wake hao kunako dakika ya 46. Ligi daraja la kwanza Taifa inashirikisha timu 16 na sasa inaongozwa na JKU yenye pointi 34.

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi