loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dada bado upo upo?

Mimi nipo byee, hali yangu burudani, Jumapili ndiyo hiyoo inayoyoma, ilikuwa Januari sasa Novemba, kila kukicha siku za kuishi zinapungua, usijisahau, hatujui siku wala saa.

Alhamisi iliyopita nilipata nafasi ya kusikiliza kwa makini wimbo wa Mwana Falsafa, Bado nipo nipo tu, naamini mashairi yake bado yanagusa vijana wengi hususan wale wasiotaka ‘kuhalalisha’ yale mambo yetu yalee!

Baada ya wimbo ule kumalizika, niliutafakari na kupata wazo la kuuliza upande wa pili, dada zangu mtaolewa lini? Au bado mpo mpo tu kwanza?

Mwana FA anasema, ‘wa kuoa nitakuwa mimi bwana?’ Wewe upo kwenye kundi la wenye mtazamo kuwa ‘wa kuolewa utakuwa wewe?’

Wakati naandika haya dada mmoja alikuja nilipokuwa nimekaa ofisini, nikamuuliza ataolewa lini? Akanijibu hana hata wazo la kufunga ndoa kwa kuwa anajua akifanya hivyo ataachika!

Sikumdadisi zaidi kwa kuwa aliondoka ila nilijiuliza kwa nini awe na uhakika wa kuachika? Au kwa kuwa hatoki Tanga yalipozaliwa mapenzi? Au hutaki kucheza kamari? Hutaki kulia, unaogopa kuja kuhurumiwa?

Wewe huolewi kwa sababu unaogopa uchungu waliopata/wanaopata wenzio kwenye ndoa? Au umewahi ‘kutendwa’ hutaki kuumizwa tena?

Mwana FA anasema haoi kwa sababu hataki kuibiwa, wewe je? Au na wewe unasubiri uzeekezeeke ndiyo uolewe?

Nakuuliza haya kwa sababu ndiyo hali halisi, kijana mwenzenu kasema haoi kwa sababu akiona mwenzake anaibiwa anaona kama anaibiwa yeye, wewe vipi?

Hujaona mwanamume wa kukuoa? Au na wewe unaamini kuwa wanaume wana wapenzi wao wa zamani kwa hiyo hutakuwa peke yako?

Au na wewe ni kama wale wanaofikiria fedha zaidi kuliko mapenzi? Sitaki kuamini eti kuna wanaume wanaouzana!

Kwani ni kweli ukitaka awe mwanamume wako peke yako labda umuumbe mwenyewe? Bila shaka pia wewe si kama wale wenye visasi, ukiibiwa na wewe unatafuta mnyonge unamuibia.

Naamini wewe sio kama wale wenye bahati mbaya kama wanalala na bundi, kwa nini usijipe moyo, hujiamini? Unasita kujitia maufundi?

Hivi na wewe unaamini kuwa kuna vibinti vidogo vinavyoweza ‘kumhifadhi’ mumeo? Kwani kuna wanaume wanaotoroka na Wazungu, na ‘kumegwa’ na mijimama?

Unaogopa kuibiwa au kukimbiwa? Au hupendi mwanamume, unapenda mwanamume handsome, kwani si kuna wanaume ‘wa kawaida’ wanaojiheshimu hata kama hawana magari?

Wasio na uwezo wa kuhonga hati za nyumba au kugeuzwa ATM?

Sasa kama si hivyo unaolewa lini? Au bado upo upo tu kwanza? Samahani kwa kukuchosha kwa maswali, sasa nisingekuuliza leo ulitaka nikuulize lini? Ni hayo tu, kuwa mwangalifu.

Waziri Mkuu Mstaafu, ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi