loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dar yatoa milioni 7/- kwa wajasiriamali

Hayo yalisemwa na Ofisa Maendeleo wa Jiji, Magreth Mazwile wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa vikundi hivyo jijini.

Alisema kuwa lengo la kuwapatia mkopo huo ni kuwasaidia wajasiriamali katika kuongeza mtaji na kujikomboa na hali ngumu ya maisha.

Kundi la kwanza la wajasiriamali lijulikanalo kama Mindu Youth Group chenye wanachama tisa, walikabidhiwa Sh milioni mbili kwa ajili ya kuongeza mtaji ambazo shughuli kubwa za kundi hilo ni ufundi seremala, kutengeneza thamani za majumbani na ofisini.

Aliongeza kuwa kundi la pili kutoka Buguruni Kisiwani, la Hygiene and Technician Environment Group lenye wanachama 20 limepatiwa mkopo wa Sh milioni 2.5 ambazo zitawasaidia katika shughuli mbalimbali za usafi wa mazingira, kununua mikokoteni 20 na vifaa mbalimbali vya ofisi.

Aidha, alisema kundi la tatu kunufaika na mkopo huo Vicoba Tunaweza Group A ambalo lina wanachama 25 na walipatiwa Sh milioni 2.5, shughuli kubwa zinazofanywa na kundi hilo ni mradi wa uuzaji wa vyakula vya nafaka.

Naibu Meya wa Jiji, Zena Mgaya ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwataka wajasiriamali hao kurejesha mikopo hiyo kwa wakati kama walivyopangiwa ili waweze kuwasaidia wajasiriamali wengine akibainisha kuwa huo ni mwanzo tu na wangehitaji kuendelea kuwasaidia wajasiriamali wengine.

ASKOFU mpya wa Jimbo Katoliki Mpanda, Eusebius Nzigilwa amekumbushwa kuwa ...

foto
Mwandishi: Sophia Mwambe

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi