loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Dawa ya migogoro ya ardhi inakuja’

Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ramadhan Abdalla Shaaban alisema hayo wakati akitoa ufafanuzi na maelezo ya Kamati Teule iliyoundwa kuchunguza matukio ya migogoro ya ardhi.

Alisema Zanzibar imeibuka migogoro mingi ya ardhi katika kipindi cha miaka 20 ambayo imechangiwa zaidi na kuongezeka kwa thamani ya ardhi zaidi baada ya kuja kwa maendeleo ya Sekta ya Utalii nchini.

Shaaban alisema thamani ya ardhi imepanda zaidi yale maeneo ya Kaskazini na Kusini mwa fukwe za pwani ya Unguja kufuatia kuongezeka kwa thamani ya Sekta ya Utalii.

“Mheshimiwa Naibu Spika hivi sasa thamani ya ardhi Zanzibar imeongezeka kwa kiwango kikubwa na ndiyo chanzo cha migogoro zaidi katika maeneo ya utalii,” alisema.

Akifafanua zaidi Shaaban alisema watendaji pamoja na wananchi wenyewe kushindwa kuzifuata vizuri sheria za ardhi kumechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa migogoro ya ardhi nchini.

“Migogoro ya ardhi Zanzibar imechangiwa na mambo mengi..... kwanza wananchi hawafuati sheria za ardhi lakini pia kuongezeka kwa thamani ya ardhi kutokana na kuimarika Sekta ya Uwekezaji pia kumeongeza migogoro,” alisema.

Aliwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kusajili ardhi kwa ajili ya kuondokana na tatizo la migogoro ya ardhi.

“Zoezi la usajili wa ardhi linaendelea nchini kote ambapo wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwani ndiyo mkombozi wa kutatua migogoro ya ardhi nchini na kuweza kuwatambua wamiliki halali,” alisema.

Aidha Shaaban alisema tayari jumla ya ekari za ardhi 66,000 zimegawiwa kwa wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo Sekta ya Kilimo.

Hata hivyo alisema Serikali imesikitishwa na tabia ya baadhi ya wananchi kuuza maeneo ya ardhi ya ekari tatu tatu ambayo ni maalumu kwa ajili ya Maendeleo ya Kilimo.

“Mheshimiwa Naibu Spika tumesikitishwa sana na tabia ya baadhi ya wananchi waliopewa eka tatu tatu kwa ajili ya kazi za kilimo ambao waliamua kuuza maeneo hayo kinyume na utaratibu uliowekwa,” alisema.

Shaaban alisema eka tatu za ardhi zilitolewa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume kwa ajili ya kuwapatia wananchi kwa kazi za kilimo na maendeleo.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Khatibu Suleiman

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi