loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC akaangwa Tume ya Maadili

Mwalende ambaye ni shahidi wa tatu katika shauri linalomkabili Gamba, alidai amefanya kazi serikalini kwa miaka 24 katika utumishi wa umma, miaka saba katika Serikali Kuu na miaka 14 katika halmashauri, lakini miezi mitano aliyofanya katika wilaya hiyo hataisahau maisha yote.

Alikuwa akitoa ushahidi wa upande wa mashtaka ambao ni Sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa umma, katika Baraza la Maadili wa viongozi wa Umma lililo chini ya Mwenyekiti wake, Jaji mstaafu Hamisi Msumi kuhusu tuhuma zinazomkabili DC huyo za kutumia madaraka yake vibaya alidai kudhalilishwa na Gamba.

Alidai Mkuu huyo wa wilaya amekuwa na lugha chafu kwa viongozi wenzake, ana utawala wa mabavu bila kuzingatia kanuni na sharia, jambo ambalo ni kikwazo kwa maendeleo ya wilaya hiyo. Alidai alitukanwa mbele ya Waziri wa Maji kwa kuitwa mkurugenzi wa hovyo.

Aidha, alisema mkuu huyo wa wilaya amesababisha kukwama kwa maendeleo ya wilaya hiyo huku akiwaweka `mahabusu’ viongozi wanaofanya kazi kwa kufuata kanuni na sheria kwa kutaka kufuata maamuzi yake.

Mkurugenzi huyo ambaye amesimamishwa kazi na DC huyo na kumleta mkurugenzi mwingine ameeleza kuwa halmashauri hiyo ina wakurugenzi wawili wanaolipwa mishahara hivyo, kuongezea gharama serikali.

Alidai amesimamishwa kazi na mkuu huyo wa wilaya huku tuhuma zikiwa hazijathibitika na kupelekwa mkurugenzi mwingine, hivyo kuwa wawili na wote wanalipwa sawa.

Alidai kwa wakati tofauti amekuwa akimtukana Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kuwa mwizi na mla rushwa, ikiwa ni pamoja na kuwaambia mmoja wa watendaji wa halmashauri hiyo kuwa amepata shahada kwa kutumia nguo ya ndani.

Alidai kuwa alipotaka kutekeleza majukumu ya kumwajibisha mfanyakazi mbadhirifu aliyekuta ripoti yake wakati anaripoti ofisini hapo baada ya tume iliyoundwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kumuagiza, alimwambia suala hilo litamtokea puani.

“Kuna siku alituita mimi na Ofisa Utumishi na kutaka kumrejesha kazini mwalimu aliyekuwa hajahudhuria kazini kwa miaka mitatu tukakataa ndipo akaagiza tuwekwe rumande, lakini mimi nilikataa na kupewa askari wa kike anilazimishe lakini niliwasiliana na RCO (Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa) sikulala rumande,” alisema.

Alidai kuwa Ofisa Utumishi alilala ndani kwa siku kadhaa na yeye kufuatilia polisi, lakini aliambiwa hawezi kutoka mpaka kwa amri ya DC na baadaye diwani mmoja alifanikiwa kumtoa.

Alidai pia kuwa DC huyo alimweka ndani Mhandisi wa Maji wa wilaya na kutaka achukuliwe hatua na polisi hawakutaka kumtoa mpaka DC alipotoa kibali.

Mkurugenzi huyo alisema amefanya kazi serikalini kwa miaka 24 katika utumishi wa umma, miaka saba katika Serikali Kuu na miaka 14 katika halmashauri, lakini miezi mitano aliyofanya katika wilaya hiyo hataisahau maisha yote.

Baraza lilimtaka kuwasilisha vielelezo vya ushahidi wa sauti zenye maneno ya matusi na maandishi ya uongozi wa mabavu ambayo shahidi huyo alikiri kuwa navyo.

Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi