loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC akaribisha wawekezaji sekta ya uchimbaji madini

Kauli hiyo aliitoa kwenye mkutano wa hadhara juzi wakati alipokuwa akijitambulisha kwa wananchi katika ziara yake ya kwanza aliyoianza wilayani hapa.

Alisema ili wilaya ya Igunga iweze kusonga mbele kimaendeleo ni vema milango ikafunguliwa wazi kwa kampuni mbalimbali ambazo zinaweza kuja kuwekeza hapa kwa kuwa wilaya ya Igunga ni miongoni mwa wilaya zenye madini ya kutosha.

Alibainisha kuwa endapo kampuni hizo zitapatikana, wananchi wanaweza kupata ajira kwa kuwa nao watapatiwa fursa ya kutengewa maeneo ya wachimbaji wadogo.

Aidha amewataka wananchi wa Igunga kulima mazao ya mtama, mihogo pamoja kunde kutokana na ukame ambao ameukuta katika wilaya ya Igunga kwani endapo mazao hayo yatalimwa kwa wingi yanaweza kuondoa upungufu wa chakula katika wilaya.

Wakati huo huo, mkuu huyo wa wilaya ametenga siku maalumu ya usafi katika mji wa Igunga ambayo itakuwa ikifanyika kila Alhamisi ambapo wananchi wote watatakiwa kufanya usafi katika maeneo yao ya biashara na makazi.

Zipporah amewaagiza watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa vyumba vya maabara ili viweze kukamilika kwa muda uliopangwa.

Naye Mkurugenzi wa mamlaka ya mji mdogo wa Igunga, Pascrates Kweyamba alisema endapo wawekezaji watafika mji wa Igunga itawawezesha kupata mapato kwa wingi kutokana na vyanzo vya madini na vinginevyo.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Igunga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi