loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC ashauri Airtel kufungua maduka makubwa vijijini

Ushauri huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Norman Sigala, wakati akifungua duka kubwa na la kisasa la kampuni hiyo jijini Mbeya.

Alishauri wajenge maduka hayo maeneo ya vijijini, ambako wananchi wengi hawapati fursa ya kupata huduma kama hizo, na kudai kuwa huduma nyingi za kibenki zimejikita zaidi maeneo ya mijini pekee na itakuwa ni vyema kwa kampuni hiyo kufikisha huduma hizo vijijini kupitia Airtel Money.

“Najua uongozi wa Airtel ni sikivu sana, nawaomba duka kama hili mngefungua na maeneo ya Mbeya Vijijini, naona mengi yako mjini tu, kule vijijini huduma kama hizi hakuna, najua mmenisikiliza na natarajia matunda mazuri kutoka kwenu,” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Aliwataka pia wananchi kutumia fursa hizo ambazo ni adimu kuchochea fursa za uchumi.

Kwa upande wake Meneja wa Airtel, Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Mushi alisema wameboresha huduma mbalimbali na kuzitaja baadhi kuwa ni pamoja na huduma ya Airtel money, na nyingine ni kuwa na ushirikiano mzuri kati yao na kampuni ya Tigo.

Alifafanua kuwa kwa sasa mteja wa Tigo anaweza kupata huduma za fedha kutoka kwenye mtandao wa Airtel, na wakati huo pia mteja wa Airtel anaweza kupata huduma hiyo hiyo kwenye kampuni ya Tigo hivyo kupanua wigo wa kibiashara.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mbeya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi