loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC Dodoma akabidhi Toyota IST

Mkazi huyo wa Dodoma aliyekabidhiwa gari ni Ivan Mbogambi anayetoka Kongwa. Akizungumza katika hafla ya makabidiano ya gari yake, Mbogambi alisema: “Nina furaha kubwa leo kwani nimeweza kuwa mmoja wa watu wanaomiliki gari wilayani kwetu.

Mimi ni mkulima wa hali ya chini leo hii Airtel imeniwezesha kubadili maisha yangu kwa kunirahisishia katika nyanja ya usafiri, mimi pamoja na familia yangu.”

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Betty Mkwasa alisema, “Ninafarijika sana kuona Watanzania kutoka kada mbalimbali wakiibuka washindi wa promosheni hii. Hii inaonesha ni namna gani Airtel wamejipanga kuboresha maisha ya watanzania.

“Kingine ningependa kuwapongeza Airtel kwa kuweza kuboresha maisha ya watanzania kwani kumpatia mtu usafiri ni jambo jema sana itasaidia kuboresha maisha yake na familia yake kwa ujumla, “ alisema Betty.

Promosheni hiyo bado inaendelea na kila siku mteja wa Airtel ana uwezo wa kujishindia gari moja kila siku kwa kujiunga na Airtel Yatosha ya siku, wiki au mwezi moja kwa moja anaunganishwa kwenye droo ya Airtel Yatosha na kupata nafasi ya kujishindia Toyota IST.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi