loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

DC- Matatizo ya Muungano ni ya mpito

Hayo yalielezwa jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amina Masenza wakati wa maaadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika shule ya msingi Sengerema wilayani Sengerema.

Alisema changamoto za muungano ni fursa ya kuimarisha na si kuuvunja na kwamba huko tuendako wananchi watarajie kukutana na changamoto nyingine hata wakifanikiwa kuzikabili zilizopo leo.

Alisema pamoja na mafanikio ya muungano yaliyokwishapatikana katika kipindi cha miaka 50, bado unapitia changamoto mbalimbali zikiwemo za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

“Matatizo tuliyonayo hivi sasa ni ya mpito, tuunganishe nguvu kama taifa tuone namna tutakavyoyakabili,” alisema.

Alisema suluhisho haliwezi kuwa katika kususa vikao halali vya Bunge, kufanya mikutano isiyo halali ama kutukana waasisi wa Muungano uliodumu kwa miaka 50.

“Wana Mwanza tuwakemee wale wote wanaoshabikia uvunjifu wa amani na wanaotumia mjadala wa sasa wa uandishi wa katiba mpya kutaka kujinufaisha wao au kujipatia umaarufu wa kisiasa kwa upotoshaji wa wananchi,” alisema Masenza.

Alisema hatima ya Muungano ipo mikononi mwa wananchi hivyo wawe tayari kuulinda, kuuimarisha na kuudumisha. Hata hivyo baadhi ya wananchi waliohojiwa katika maadhimisho yao ya miaka 50 ya muungano walisema muungano unawafanya watembee popote wakiwa na amani tena bila woga.

Rosalie Suka anasema wakati Tanganyika na Zanzibar zikiungana yeye alikuwa darasa la saba na ameona mafanikio makubwa hivyo kuwaomba watanzania wenzake wazidi kuulinda na kuudumisha.

Alisema watakapolazimisha kuuvunja watakaopata shida ni wanawake na watoto kama ilivyo kwenye vita. Alisema wanasiasa wanaopinga Muungano hawaelewi umuhimu wake ama wanaelewa lakini kubwa kwao ni uchu wa madaraka na wanatambua kuwa watawapeleka wananchi pabaya.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi