loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DED Nkasi aagizwa kufuatilia fedha NFRA

Deni hiyo ni malimbikizo ya ushuru wa mahindi aliyoyanunua wakala huyo kutoka kwa wakulima wa halmashauri hiyo kwa misimu miwili ya ununuzi.

Pia kamati hiyo ilimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kimulika Garikunga kuacha mara moja desturi ya kutotenga fedha kwa ajili ya mifuko ya wanawake na vijana ambapo sasa halmashauri hiyo imelimbikiza deni hadi kufikia zaidi ya Sh milioni 332.

Pia aliagizwa kuacha tabia ya kutolipa asilimia 20 za vijijini ambapo deni sasa limefikia zaidi ya Sh milioni 59. Maagizo hayo yalitolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Felister Bura baada ya wajumbe wa kamati hiyo kupitia kwa kina mapato na matumizi ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012-13.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Peter Mizinga alikiri mbele ya kamati hiyo kuwa halmashauri hiyo imefanya kosa kutokutenga fedha katika mifuko hiyo ya makundi maalumu pia kutolipa asilimia 20 ya vijiji.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Garikunga amekiri kuwa hali ya makusanyo ya halmashauri hiyo sio nzuri pia alimwomba Mungu amsaidie zoezi hilo la ukaguzi lipite salama kwani amebakiza miezi kumi na moja astaafu.

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Namanyere

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi