loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dhamira ya Kikwete yahenyesha TPDC

Kutokana na kauli hiyo, sasa wataalamu wa ndani na nje ya nchi, wanafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi hiyo, lakini kwa kuzingatia utaalamu na usalama kwa kiwango cha juu.

Mkakati wa kuhakikisha mradi huo unakamilika mapema, unasimamiwa kwa karibu na Bodi ya TPDC ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Michael Mwanda na Menejimenti ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, James Andilile.

Akitoa ahadi kwa Watanzania juzi, Mwanda alisema sasa ujenzi wa bomba hilo la gesi na miundombinu yake utakamilika Desemba mwaka huu, kutokana na kuwa katika hatua za mwisho kwa wastani wa zaidi ya asilimia 92.

Chini ya mkakati huo, Watanzania sasa watashuhudia gesi kutoka baharini katika Kijiji cha Madimba mkoani Mtwara, ikiungana na gesi inayotoka katika Kisiwa cha Songosongo, Lindi, ikipita kwa majaribio katika bomba hilo lenye urefu wa kilometa 542 Januari mwakani.

Juzi Bodi na Menejimenti ya TPDC, walifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kuanzia Kituo cha Kinyerezi, Dar es Salaam hadi Somanga, Kilwa na Madimba, Mtwara na kuridhishwa na kasi na ubora wa ujenzi wa mradi huo.

Meneja wa Kampuni ya Gesi ya Taifa (Gasco) iliyo chini ya TPDC, Kapuulya Musomba, aliwahakikishia wajumbe hao wa Bodi na Menejimenti ya TPDC kuwa mradi huo, utakamilika Desemba na gesi ya nitrogen itapitishwa kwa majaribio ndani ya bomba hilo Januari.

Rais Kikwete akiwa nchini Marekani miezi michache iliyopita, alisema kitendo cha gesi kuanza kuchimbwa, kuchakatwa na kusafirishwa katika bomba hilo, kitaifanya Tanzania kukuza uchumi wake kutoka wa chini kwenda wa wakati ifikapo mwaka 2025.

Mbali ya kuinua uchumi, Rais Kikwete alisema hatua hiyo itamfanya kuwa Rais wa mwisho kuiongoza Tanzania ikiwa masikini, kwani Marais watakaomfuatia wataikuta nchi ikiwa na miradi imara ya kiuchumi, itakayochochewa na upatikanaji wa nishati hiyo ya gesi.

“Napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa ujenzi wa bomba, ujenzi wa vituo vya kupokea, kuendeshea, kusafishia gesi, lakini pia ujenzi wa mageti (valve station) vyote vipo katika hatua ya mwisho kwa zaidi ya asilimia 95,” alisemaMusomba kwa wajumbe wa Bodi ya TPDC.

Andilile aliwaeleza wajumbe wa bodi hiyo, kwamba menejimenti yake itasimamia kwa karibu kila hatua ya utekelezaji wa mradi huo ili uweze kukamilika na kuanza kazi haraka kama ilivyolengwa.

Wajumbe wa Bodi hiyo walipita na kukagua miundombinu mbalimbali ya ujenzi wa mradi huo napia walijionea kujengwa kwa kiwango cha juu cha mitambo ya mradi huo, yakiwemo mageti 16 ya kuruhusu au kufunga gesi kupita, saba kati yake yakiwa yenye teknolojia ya hali ya juu.

Mageti hayo yaliyojengwa katika maeneo mbalimbali kuanzia Mtwara hadi Dar es Salaam, yataendeshwa moja kwa moja kwa mitambo iliyopo Kinyerezi, Dar es Salaam kwa kufungwa au kufunguliwa, hasa pale inapotokea majanga kama ya milipuko au ukarabati unapofanywa.

Kutokana na juhudi hizo, Mwanda alipongeza menejimenti na wafanyakazi wa TPDC kwa kuonesha uzalendo wa hali ya juu katika utekelezaji wa mradi huo, ambao alisema ni roho ya Taifa.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza, Mtwara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi