loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DIRA ya taifa ya madini yaandaliwa

Inakusanya maoni ya wadau mbalimbali lengo likiwa ni kuandaa rasimu ya kutengeneza dira ya taifa ya madini.

Akizungumzia utafiti huo ulioanza kwa Mkoa wa Morogoro, Mratibu wa utafiti huo, Ian Shanghvi, alisema kwa sasa taifa linategemea dira ya madini ya Bara la Afrika.

Dira hiyo inayotegemewa sasa, inatajwa kwamba ni kubwa kiutekelezaji na kwamba ndiyo maana sasa wanalenga kuipa thamani sekta ya uchimbaji wa madini kwa kuwa na dira ya taifa inayojitegemea.

Alisema utafiti unafanyika katika mikoa 14 na baadaye wataendelea katika mikoa mingine nchini.

Kiongozi wa utafiti huo, Margaret Kasembe, alisema Mkoa wa Morogoro unaongoza kwa kuwa na aina mbalimbali za madini, ikiwemo rubi na dhahabu.

Alisema kuwapo kwao mkoani humo, ni fursa kwa wadau wa madini kuchangia nini kifanyike katika kuupa thamani uchimbaji wa madini kwa kutumia dira ya taifa itakayopatikana.

Aidha alisema Watanzania wana nafasi kubwa ya kukuza uchumi wa nchi kwa kupitia sekta ya madini, ambapo alisema kuwa ni wakati sasa kwa wadau kutoa maoni yao kwa kujibu madodoso yenye maswali yatakayotumika kufanikisha utafiti huo.

Wadau mbalimbali wakiwemo wachimbaji na wafanyabiashara wa madini, wawakilishi wa Serikali, madhehebu ya dini na asasi zisizo za kiserikali walijitokeza kuwasilisha maoni juu ya mambo mbalimbali, yatakayosaidia kufanikisha utafiti huo.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Agnes Haule, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi