loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Bilal ahimiza wanawake vijijini kutumia huduma za afya

Dk Bilal alisema hayo katika Kijiji cha Ghana, Jimbo la Uzini Wilaya ya Kati Unguja wakati akifungua Kituo cha Afya ambacho kitakuwa kikitoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo.

Alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado haijafanikiwa kuyafikia malengo ya kupunguza vifo vya akinamama na watoto kwa sababu wanawake wengi hawana mwamko wa kuzitumia huduma za afya zaidi wakati wanapokuwa wajawazito.

“Tanzania imo katika kutekeleza Malengo ya Milenia ambayo ni kupunguza vifo vya akinamama vinavyotokana na uzazi na njia pekee ya kuondosha tatizo hilo ni kuchunguza afya hizo katika hatua ya awali...malengo hayo hatujayafikia kwa sababu wanawake wengi hawazitumii huduma hizo kikamilifu,” alisema.

Aidha, alisema amefurahishwa katika hospitali hiyo huduma za mafunzo ya darasa kwa wananchi mbalimbali ikiwemo wajawazito zitatolewa mara kwa mara.

Alisema wakati umefika kwa akinamama pamoja na wagonjwa mbalimbali kupewa darasa ambalo litasaidia kuweza kupambana na maradhi mbalimbali ambayo yamekuwa yakisababisha vifo vya wananchi kwa ujumla.

Aidha, Dk Bilal aliahidi kutoa Sh milioni 20 ili kusaidia miradi miwili ya hospitali za Jimbo la Uzini ikiwemo Hospitali ya Mpapa ambayo ipo katika hatua za mwisho za kukamilika kwa ujenzi wake.

Awali, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Abdul Jamala alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya Sekta ya Afya ambapo sasa vipo jumla ya Vituo vya Afya 139, Unguja na Pemba.

Alisema vituo hivyo kwa kiasi kikubwa vimekuwa vikitoa huduma za afya kwa wananchi mbalimbali katika hatua za mwanzo, ambapo kipaumbele cha kwanza kimewekwa kwa wananchi wa vijijini wakiwemo wajawazito na watoto.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi