loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Mukangara ataka chess ichezwe shuleni

Mwito huo ulitolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara wakati alipozungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mchezo huo nchini Dar es Salaam juzi.

Pia hafla hiyo ilihudhuriwa na bingwa wa zamani wa chess ambaye pia ni mmiliki wa Taasisi ya Kasparov Chess, Garry Kasparov.

Dk Mukangara alisema mchezo huo unasaidia kuimarisha uelewa wa wanafunzi shuleni, hivyo ni vema hata nchini, ukatumiwa katika shule mbalimbali.

Alisema kwa upande wake, yupo tayari kusaidia maendeleo ya mchezo huo nchini kwa kuwa ni moja kati ya michezo ya ndani ambayo inahitaji kutangazwa.

“Chess ni mchezo wa aina yake ambao kumbe ukitiliwa mkazo unaweza kuleta mabadiliko katika elimu nchini kwa maana kuwa wanafunzi wanaweza kuucheza na hivyo kujikuta pia wakijiimarisha zaidi kiuelewa,” alisema Dk Mukangara.

Alimwomba Kasparov kupitia taasisi yake kuendeleza mchezo huo nchini. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania, Geoffrey Mwanyika alisema tayari chama hicho kimekubaliana na Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert kuanza kujifunza mchezo huo.

Mwanyika alisema chama hicho katika kuhakikisha mchezo huo unafundishika katika shule nyingi nchini, kimeanza utaratibu wa kuwafundisha watu watakaokuwa na jukumu la kuwafundisha wanafunzi shuleni.

Alisema ili kufanikisha azma hiyo kuna kila sababu ya wadhamini mbalimbali kujitokeza kudhamini jitihada za chama hicho katika kuuendeleza mchezo huo.

“Ili kutimiza ndoto zetu peke yetu hatuwezi kabisa hivyo basi ni vema wadau mbalimbali wakatuunga mkono katika jitihada zetu hizi kwa kuwa kwanza seti moja ya mchezo huo sio chini ya dola tano, na tunahitaji kuwa na vifaa hivi vingi,” alisema Mwanyika.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi