loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Mvungi bado hajapata fahamu

Akizungumza na HabariLeo Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa MOI, Jumaa Almasi alisema hali ya mwanasiasa huyo pamoja na kuimarika ,bado si nzuri kwa kuwa bado hajapata ufahamu vizuri.

“Anaendelea vizuri tofauti na alivyoletwa hapa siku ya kwanza, ingawa bado yupo chini ya uangalizi maalum na yupo ‘unconscious’ (hana fahamu),” alisema Almasi.

Alisema madaktari wanafanya kila wawezalo, kurejesha afya yake, ambapo amechukuliwa vipimo vya CT scan ili kuweza kujua athari alizopata kutokana na majeraha aliyopata.

Wakati mwanasiasa huyo akipigania maisha yake hospitali, Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Saalam juzi lilisema linashikilia watu sita, wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo la kumvamia Dk Mvungi.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova, alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika msako wa Polisi katika maeneo ya Mpigi Magohe mpakani mwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani baada ya tukio hilo lililotokea juzi usiku.

Dk Mvungi alivamiwa nyumbani kwake na watu sita wanaodhaniwa kuwa majambazi majira ya saa saba usiku, ambao pamoja na kumpiga na kumjeruhi vibaya pia, walimuibia kompyuta mpakato moja aina ya HP, simu mbili za mkononi na fedha taslimu Sh milioni moja.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi