loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Myles Munroe kutembelea Tanzania

Akizungumza na gazeti hili katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya ziara hiyo ya Dk Munroe nchini, Thomas Massamu alisema Dk Munroe atakuwa na mkutano muhimu na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu hapa nchini katika ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Katika mkutano huo, Dk Munroe ataelezea nafasi ya vijana katika mazingira ya kisiasa na kijamii, na kuwaeleza namna ambavyo wanaweza kuwa mawakala wa mabadiliko.

Kabla ya kuondoka, Dk Munroe atafanya mkutano juu ya masuala ya uongozi ambao utahusisha wafanyabiashara, viongozi wa Serikali pamoja na wanasiasa.

Mwenyekiti wa mradi wa Dk Munroe nchini, Stella Matte alisema Dk Munroe amekuwa akisafiri duniani kwa ajili ya kuzungumzia masuala muhimu yanayogusa binadamu.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi