loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Salim azindua kazi za Profesa Haroub Othman

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha mkusanyiko wa kazi za Othman, Salim alisema msimamo wake kuhusu muungano ulikuwa wazi na tofauti na watu wanavyoelezea.

“Haroub (Othman) alikuwa akiona fahari kuwa Mtanzania na kamwe hakuidharau Zanzibar, alikuwa muumini wa muungano wa serikali mbili,” alisema.

Akizungumza kitabu hicho, Mke wa Marehemu Othman, Profesa Saida Yahya Othman alisema kitabu hicho chenye jina la ‘Yes in My Lifetime’ kinajumuisha makusanyo ya hotuba, makala na mihadhara aliyotoa wakati wa uhai wake kuanzia mwaka 1974 hadi mwaka 2009.

Alisema makala zilizomo ndani ya kitabu zinazungumzia mapambano dhidi ya ubeberu, kupitia mshikamano wa wapigania haki za wanyonge kote duniani na muungano wa Tanzania. “

Kitabu hiki ni muhimu katika jamii yetu ambamo historia inakuwa kama ukoma, tunafikiri ukombozi wetu utakuja kwa kuwaiga wengine bila ya kuhoji, tunafikiri utaifa ni chuki dhidi ya waliokuwa tofauti na sisi na uzalendo uchwara,”alisema.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi