loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Shein asifia uhusiano Z’bar, Msumbiji

Dk Shein aliyasema hayo alipozungumza na mgombea Urais wa Msumbiji kupitia chama cha Frelimo, Filipe Jacinto Nyusi, Ikulu mjini hapa jana.

Alimueleza Nyusi kuwa urafiki kati ya Serikali na wananchi wa Tanzania na Msumbiji umekuwa wa mafanikio makubwa na pande hizo hazina budi kushukuru jitihada za waasisi wa nchi hizo kwa kujenga mazingira ya urafiki wenye manufaa kwa wote.

Alibainisha kuwa mafanikio ya ushirikiano huo yamejidhihirisha pia katika ushirikiano wa nchi hizo katika ngazi za kikanda na kimataifa katika masuala mbalimbali yakiwamo ya kisiasa, kidiplomasia na uchumi.

Dk Shein alimueleza Nyusi kuwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla zinatambua jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo zilizofanywa na viongozi wa Msumbiji, kuanzia Rais wa Kwanza hayati Samora Machel hadi wa sasa, Rais Armando Guebuza.

Katika mazungumzo hayo, Dk Shein alimpogeza Nyusi kwa kuteuliwa na Frelimo kugombea nafasi ya urais wa Msumbiji na kueleza kuwa ushindi wake ni muhimu katika kujenga mustakabali wa baadaye wa nchi hiyo.

Kwa upande wake, Nyusi alisema amefurahi kufika Tanzania na kupata fursa ya kuonana na viongozi wa Serikali akiwamo Rais Jakaya Kikwete pamoja na kupokelewa kwa upendo mkubwa na viongozi na wananchi.

Alisema ziara yake ni ya kujitambulisha lakini pia kueleza matumaini yake kuwa Msumbiji na Tanzania zitaendelea kuwa ndugu na kuimarisha uhusiano wao kwa kuongeza ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchumi.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora wa SMZ, Dk Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, George Mkuchika na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi