loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Dk Shein asifu Benki ya Dunia kunufaisha Zanzibar

Dk Shein alisema hayo wakati alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji Mwendeshaji wa taasisi hiyo, Sri Mulyani Indrawati mjini hapa. Ujumbe wa Benki ya Dunia ulitembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na taasisi hiyo.

Dk Shein alisema amefurahishwa na misaada ya benki hiyo kwa upande wa Zanzibar ambayo imelenga zaidi kuimarisha miundombinu na huduma za jamii kwa ujumla.

Alisema upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume, ujenzi ambao unaendelea kwa sasa, huduma za maji safi na salama pamoja na mradi mkubwa wa kuimarisha sekta ya elimu, ni sehemu ya misaada hiyo.

“Sekta ya Elimu imepiga mafanikio makubwa ya ujenzi wa shule 19 za sekondari ambazo zimepunguza tatizo la uhaba wa nafasi kwa wanafunzi…tatizo kubwa kwa sasa ni uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi,” alisema Shein.

Kuhusu tatizo la uhaba wa ajira kwa vijana, Dk Shein alikiri na kusema ni kubwa ambalo sekta ya utalii ndiyo tegemeo la kutoa ajira kutokana na kupiga hatua kubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa hoteli zenye hadhi ya juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia aliahidi kusaidia Zanzibar katika juhudi zake za kupambana na umasikini kupitia Mpango wa Mkuza na Dira ya Maendeleo ya 2020.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi