Dk Shein aliyasema hayo leo alipofanya mazungumzo kati yake na Balozi wa Marekani nchini, Mark Bradley Childress aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Katika maelezo yake, Dk Shein alimweleza Balozi Childress kuwa jitihada kubwa zimefanyika katika kutekeleza miradi ya MCC hapa nchini na kuweza kupata mafanikio makubwa, hivyo ni imani yake kubwa kuwa awamu ya pili ya mfuko huo itaendelezwa.
Naye Balozi Childress alipongeza mafanikio yaliyopatikana hapa nchini kupitia ufadhili wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) awamu ya kwanza.