loader
Dstv Habarileo  Mobile
Dk Slaa afunda madiwani Nzega matumizi ya bil.2.3/-

Dk Slaa afunda madiwani Nzega matumizi ya bil.2.3/-

Dk Slaa alisema hayo hivi karibuni katika mkutano wa hadhara, uliofanyika katika viwanja vya Parking, mjini Nzega.

Katibu huyo alisema pesa hizo za ushuru wa huduma kutoka Resolute kiasi cha Sh bilioni 2.3, zitumike katika ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kupunguza kero kwa wananchi wa maeneo husika.

Akihutubia mamia ya wananchi wa Nzega, alisema kiasi kingine cha pesa kianzishe benki ya kijamii, itakayowawezesha wananchi kukopa na kuboresha uchumi wa wilaya ya Nzega na wananchi kwa ujumla.

Baraza la madiwani lililopita halikuridhia matumizi ya pesa hizo huku baadhi ya madiwani, walidai pesa hizo zigawanywe kwa kila kata. Madiwani wengine waliamua pesa hizo zinunue mitambo ya ujenzi wa miundombinu katika halmashauri hiyo.

Mzozo mkubwa ulitokea katika baraza hilo hadi kushindwa kufikia maamuzi ya matumizi ya fedha hizo. Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Patrick Mbozu aliridhia kuwa Baraza Maalumu litajadili matumizi stahiki ya fedha hizo.

Awali, mgodi wa dhahabu wa Resolute uliilipa halmashauri ya wilaya Sh bil. 2.3 kama ushuru wa huduma. Fedha hizo hazijatumika huku baadhi ya wananchi wakitegemea maamuzi na matumizi stahiki, yatakayonufaisha wananchi wote wilayani humo.

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi