loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Drogba- Nipo tayari kurudi Chelsea

Drogba, ambaye aliisaidia Chelsea kutwaa ubingwa wa Ulaya kabla ya kwenda China kujiunga na Shanghai Shenhua ya huko mwaka 2012, leo anatarajia kuungana na klabu yake ya zamani wakati the Blues itakapokuwa mgeni wa Galatasaray mjini Istanbul kwenye mechi ya kwanza ya mtoano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anamaliza mkataba wake msimu huu na alipoulizwa na Daily Mail kama anaweza kurudi kwenye Ligi Kuu, alisema: “Kama itakuwa hivyo basi ni kwa timu moja tu.

“Mkataba wangu unakwisha msimu huu kisha nitafanya uamuzi kipi ni bora kwangu, lakini nilikuwa na wakati mzuri sana Chelsea na kama Jose atasema 'Didier nataka urudi', nitafikiria hilo," alisema.

Aidha, alisema kwenye The Sun: “Hakuna klabu yoyote iliyonifuata kwa hiyo hatuwezi kulizungumzia hilo, maana ni tetesi tu".

Drogba, alifunga mabao 157 alipokuwa Chelsea tangu aliposajiliwa kutoka Marseille mwaka 2004, amekuwa akizungumziwa kwamba anaandaliwa kuwa kocha mchezaji Stamford Bridge na pia imeripotiwa ana ofa kama hiyo katika klabu ya Ligi ya Marekani, MLS, lakini ameiambia BBC kwamba huenda akaendelea kuishi Uturuki. Alisema:

“Nitaangalia kila ofa kipindi cha usajili, lakini nitaangalia zaidi itakayotoka Galatasaray kwa sababu wamenipa nafasi nyingine ya kucheza kwa kiwango kikubwa, nitaona kitakachokuwa mezani, nataka kushinda sio kucheza tu, lakini kucheza na kushinda".

Aliongeza: “Nina furaha sana Galatasaray na mashabiki wamekuwa wazuri kwangu, tulishinda taji la ligi ya Uturuki msimu uliopita na kuiondoa Juventus hatua za mwanzo za Ligi ya Mabingwa.

“Lakini sijafika mwisho na Chelsea na sitaki hilo litokee, watu wanafahamu jinsi ninavyoipenda klabu ile na mashabiki, sitasahau niliyoyafanya nikiwa pale na kumbukumbu zote Chelsea, siku zote ina nafasi maalumu kwenye moyo wangu na maisha yangu".

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi