loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DUCE yapokea wanafunzi 200 badala ya 500

Mkuu wa chuo hicho, Profesa David Mfinanga alimueleza hayo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Mhagama alipotembelea kujionea miundombinu ya Mradi wa Sayansi Teknolojia na Elimu ya Juu (STHEP) ulio chini ya wizara hiyo kwa nia ya kukuza elimu ya juu nchini.

Alisema hatua hiyo ni mafanikio ya mradi huo uliowezesha chuo kupata vitabu na sasa wanafunzi wanne wanatumia kitabu kimoja badala ya awali kitabu kimoja kwa wanafunzi 20.

Alisema pia walimu kadhaa wa chuo hicho wanasomeshwa katika ngazi ya PHD. Profesa Mfinanga alisema kupitia mradi wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), wanatarajia kupata wanafunzi zaidi, kwani kwa sasa wamefanikiwa kuwa na maabara za kisasa kwa masomo yote ya Sayansi na kuhamasisha watoto wa kike kujitokeza kusoma masomo hayo.

Kwa mujibu wa Profesa Mfinanga, kwa sasa wana wanafunzi wa kike wanaosoma sayansi katika chuo hicho hawazidi 15. Profesa Mfinanga alisema katika mwaka huu wa fedha, wanaanza kutoa mafunzo mtandao kwa mwaka mmoja kwa walimu waliopo kwa ngazi ya diploma ya uzamili katika elimu ili kuwezesha walimu wengi walioko kazini kupata elimu hiyo.

Baada ya kumaliza ziara chuoni hapo, Naibu Waziri alikipongeza chuo hicho kwa kukamilisha miradi hiyo kwa kiwango cha juu na kutaka kutumia vyema miundombinu hiyo kwa kuikarabati mara kwa mara ili kulinda uwekezaji huo mkubwa wa serikali na kuleta mabadiliko ya sekta ya elimu.

Mbali na chuo hicho, pia mradi huo ulitekelezwa katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Mkwawa (MUCE), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Serikali cha Zanzibar (SUZA).

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi