loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EAC yakana kupokea barua ya Waziri Sitta

Wiki iliyopita,Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta aliliambia Bunge kuwa Tanzania imeandika barua Makao Makuu ya EAC jijini Arusha, ikitaka ufafanuzi wa ushirikiano wa nchi hizo tatu na kwamba majibu yatapatikana baada ya wiki mbili.

Majibu ya barua hiyo,kwa mujibu wa Sitta, ndiyo yangeipa Tanzania hatua za kuchukua baada ya nchi hizo tatu wanachama wa Jumuiya hiyo kati ya tano kudhiihirika kuvunja mkataba kwa kuzitenga Tanzania na Burundi katika masuala yanayohitaji uamuzi wa nchi zote wanachama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu Mkuu wa EAC,Dk Richard Sezibera alisema hadi jana alikuwa hajapokea barua yoyote kutoka Tanzania kuhusu mgogoro huo, unaofukuta chini kwa chini.

“Sijapokea barua yoyote kutoka Tanzania kuhusiana na suala hilo na ufafanuzi wa ushirikiano wa nchi hizo tatu utatolewa katika kikao kijacho cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya kitakachofanyika baadaye mwezi huu,”alisema Dk Sezibera baada ya kuulizwa.

Alipobanwa zaidi juu ya ushirikiano huo, Dk Sezibera alisema kuwa nchi hizo zimeamua kuharakisha utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyokubaliwa na nchi wanachama, maamuzi aliyodai kufikiwa mwaka 2004.

Hata hivyo, uamuzi wa mwaka 2004 ulihusiana na kuharakishwa kwa shirikisho la kisiasa la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Tume iliyokuwa ikiongozwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Amos Wako ilikusanya maoni ya wananchi ambao wengi wao walipinga kuharakisha uundaji wa shirikisho la kisiasa.

Dk Sezibera alikuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Serikali ya Sudan Kusini, ambayo imeomba kuwa mwanachama wa Jumuiya hiyo yenye nchi tano wanachama.

Kiongozi wa Ujumbe huo,Aggrey Sabuni ambaye ni Waziri wa Fedha na Uchumi wa Sudan Kusini, alisema wameomba kujiunga na EAC kutokana na sababu za kihistoria na ushirikiano wa muda mrefu miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo na Afrika Mashariki.

RAIS John Magufuli amesema Manispaa ya Ilala imepandishwa ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi