loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ebola wadaiwa tishio kwa uchumi

Taasisi hiyo ya fedha imesema kuwa, iwapo kasi ya kuenea virusi vya ugonjwa huo haitazuiwa, hadi mwishoni mwa mwaka huu, ebola inaweza kusababisha hasara ya mabilioni ya dola katika uchumi wa nchi za Afrika Magharibi.

Hayo yanajiri huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kufanya kikao cha dharura kujadili mfumuko wa ugonjwa huo.

Inatarajiwa kuwa kutapitishwa azimio la kuitaka jamii ya kimataifa ifanye jitihada zaidi za kukabiliana na maradhi hayo, na nchi kutakiwa kusaidia maofisa wa tiba na wataalamu wa hospitali.

Mfumuko wa sasa wa ebola umesababisha maafa makubwa zaidi tangu ugonjwa huo ulipogunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976.

Wakati hayo yakibainika, Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa, dola bilioni 1 zinahitajika kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa ebola katika nchi za Afrika Magharibi ambao unahofiwa kugeuka kuwa janga la kibinadamu iwapo jitihada za kimataifa hazitochukuliwa.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Bruce Aylaward alisema, idadi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa huo bado inaongezeka na kwamba ni vigumu kutoa makadirio sahihi kuhusu idadi ya watu wanaoweza kuambukizwa virusi vya ebola.

Hayo yanajiri huku Marekani ikisema kuwa itaongoza jitihada za kupambana na ugonjwa wa homa ya ebola huko Magharibi mwa Afrika.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: WASHNGTON, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi