loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Elimu duni ya kondomu yachagiza maambukizi mapya ya VVU

Pamoja na dai hilo wanasema kwamba kondomu inapunguza nguvu. Kutokana na dhana hiyo potofu wataalamu wanasema kunakuwapo na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi miongoni mwa vijana.

Hayo yameelezwa na Ofisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/Ukimwi kutoka Unesco, Herman Mathias wakati akiwasilisha mada katika warsha kwa washauri wa Vikundi vya Vijana na wasikilizaji wa masuala ya kuzuia maambukizi ya VVU na Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-17 ambao ni walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio.

Katika warsha hiyo ya siku mbili inayoendeshwa na UNESCO kwa kushirikiana na UNICEF katika kituo cha Redio cha Nuru FM Iringa, Mathias amesema kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu sahihi kwa vijana ya kujikinga na maambukizi ya VVU na mimba kutokana na uelewa mdogo wa vijana katika matumizi sahihi ya kondomu.

Wakichangia mada kuhusu masuala muhimu yanayowahusu vijana katika maambukizi ya VVU vijana wamesikitishwa na mimba za utotoni kwa wasichana zinazochangia vifo vya mama na watoto na wasichana kuacha masomo.

Washiriki wa warsha hiyo wametaka hatua za haraka zichukuliwe kuhakikisha kuwa sheria za mtoto zinazoruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo zinafanyiwa marekebisho ya haraka kulinda haki ya mtoto wa kike.

Akitoa mada kuhusu mbinu mbalimbali za kuwezesha majadiliano katika vikundi vya wasikilizaji, Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Abdul Mfuruki amewataka wawezeshaji kutumia nafasi walizonazo kuendesha mjadala wenye tija.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi