loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Elimu ya gesi yahitajika’

Changamoto hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa TEWW, lililokutana mjini hapa.

Kwa mujibu wa Bendera, katika kutoa mafunzo ya elimu katika mfumo usio rasmi uliowafikia watu wengi hasa waishio vijijini, TEWW haina budi kushirikiana na vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi, katika kuandaa programu hizo zitakazokidhi soko la ajira hasa katika uchumi mpya wa gesi.

Mkuu huyo wa Mkoa, alisema kuanzishwa kwa elimu ya masafa ya kozi za nishati na gesi, kutasaidia watu wengi wenye sifa kujifunza na wahitimu wake watanufaika katika soko la ajira nchini, sambamba na kupunguza umasikini.

Alisema hivi sasa nishati ya gesi ya kutosha imegunduliwa na inahitaji wataalamu wengi wa aina mbalimbali, hivyo kuanzishwa kwa elimu hiyo kutasaidia kuongeza ajira kwa Watanzania. “

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ina jukumu kubwa la kubuni kozi zake ikiwemo ya nishati ya gesi, ili kutoa vijana wengi kuingia katika soko la ajira na kupunguza umasikini,” alisema.

Mwenyekiti wa baraza hilo, Edward Rugakingira, alisema kikao hicho cha baraza kinafanyika kwa ajili ya kuchambua changamoto mbalimbali na kuziwekea mikakati, ili kuboresha utendaji wa kazi katika siku za usoni.

Hata hivyo alisema, baraza hilo limekuwa likikutana mara moja kwa mwaka kushauri Menejementi jinsi ya kuendesha kwa ufanisi taasisi, bila kuwepo kwa migongano ndani yake.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi