loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EPZA kuanzisha kituo cha wawekezaji wa gesi

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk Adelhelm Meru aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa hatua hiyo ni muhimu katika undelezaji wa eneo huru la bandari ya Mtwara. EPZA inaendeleza hekta 10 za eneo huru la bandari ya Mtwara.

Hekta hizo ni kati ya jumla ya hekta 110 za eneo hilo huru la bandari ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji mbalimbali. Eneo hilo litaendelezwa kwa kuwekewa miundombinu inayotakiwa na kisha kugawiwa kwa kampuni za kimataifa zinazofanya kazi za kutoa huduma mbalimbali kwa kampuni zinazofanya kazi ya utafiti wa mafuta na gesi katika Mkoa wa Mtwara.

Alisema kituo hicho cha huduma kwa kampuni zinazofanya utafiti wa gesi na mafuta mkoani Mtwara, kitakuwa cha kipekee si kwa Tanzania pekee bali katika ukanda mzima wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.

“Leo tunahitimisha safari ndefu ya uanzishaji kituo kipya katika bandari huru ya Mtwara ambacho kitahudumia watafiti wa gesi na mafuta,” alisema.

Alisema kampuni hizo sasa zitaenda kuanzisha karakana kubwa kwa ajili ya kuzihudumia kampuni mbalimbali zikiwemo British Gas na Start Oil zinazofanya kazi ya kutafiti gesi na mafuta katika eneo hilo.

Alizitaja kampuni zilizosaini makubaliano hayo kama Slumberger Seaco Inc ya Marekani, Altus Oil Field Supplies Services ya Singapore, Tans Ocean Industries and Services LTD ya Dubai na Lenna ya Iran.

Alisema kampuni hizo ni kubwa na zina uzoefu mkubwa wa shughuli hizo na zimepatiwa maeneo katika eneo la hekta 10 kuanza kujenga na kutoa huduma.

“Katika eneo hili watajenga karakana kubwa kwa ajili ya kufanyia ukarabati na matengenezo ya vifaa vya mafuta na gesi,” alisema.

Alifafanua kuwa karakana hizo zitajengwa za kisasa na zitakuwa na uwezo pia wa kuhudumia nchi jirani kama Kenya, Msumbiji, na Afrika Kusini.

Meneja Mradi Mwandamizi wa Kampuni ya Altus Oil Field Supplies Services Singapore, aliyefahamika kwa jina moja la Sankaranarayanan, alisema kampuni yake imejiandaa kuanza kufanya kazi ya kutoa huduma kwa kampuni za utafutaji gesi na mafuta.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi