loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EPZA yataka Waturuki kuanzisha viwanda nchini

Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dk Adelhelm, Meru alisema hayo leo wakati akizungumza katika maonesho ya kimataifa ya bidhaa mbalimbali kutoka nchini Uturuki.

Dk Meru alitaka kampuni za Uturuki zifikirie kuwekeza nchini haswa katika viwanda vya uzalishaji, hususani katika viwanda vya nguo, ili Watanzania wengi wanufaike na teknolojia waliyonayo.

“Fikirieni kuwekeza na kujiimarisha katika viwanda vya uzalishaji…Watanzania wanahitaji kupata faida, teknolojia pamoja na kukuza uchumi wetu,” alisema Dk Meru na kuongeza kuwa ingawa ziko kampuni chache kutoka Uturuki hapa nchini, lakini waongeze wigo.

Akifungua maonesho hayo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk Reginald Mengi alisema kupitia maonesho ya Waturuki, Watanzania wajifunze kupitia bidhaa hizo kwa kuwa na ubora na bei rahisi.

Alisema Watanzania wanahitaji kujifunza ujuzi kutoka Uturuki na kuutumia katika kuzalisha bidhaa zao na kuwa bora zenye kukubalika.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi