loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EU yaahidi kusaidia ukuzaji kilimo

Akiwa katika skimu hiyo inayosaidiwa na Shirika la Chakula Duniani (FAO) ametaka miradi ya maendeleo nchini kutowaacha nyuma wanawake na watoto kwani wao ndio msingi wa maendeleo ya kijamii kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.

Balozi huyo ambaye anatarajiwa kurejea Ulaya mwaka huu, baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini amesema kwamba kuwapo kwa asilimia 60 ya wafaidika na mradi huo wa mpunga kuwa wanawake kumesaidia sana kuhamasisha maendeleo ambayo yanatakiwa kuendelea kusimamiwa.

“Wanawake wamefanikiwa kupeleka watoto wao shuleni, kuwapatia chakula kinachostahiki na kupata kipato na katika hili ni vyema wasiachwe nyuma kimaendeleo,” alisema balozi huyo.

Mradi wa Kiroka ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya FAO na benki ya NMB ikishirikiana na RaboBank umelenga kuboresha kilimo cha mpunga na pia kuwawezesha wakulima hao kuwa na nafasi ya kupata fedha za kuendeleza majukumu yao.

Mradi huo ulioanza 2004 na kutarajiwa kuisha Juni mwakani unatekelezwa 2018 umelenga kufungua fursa kwa wanawake na wanaume na kuongeza uzalishaji, kusaka masoko, kupata njia ya kupata mikopo na kujenga uwezo wa kufanikisha shughuli za maendeleo kwenye skimu. Mradi huo unatarajiwa kutumia dola za Marekani 737,000 hadi utakapokamilika.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka Mbaraka amesema skimu imewasaidia kuinua maisha ya wananchi kwa kuwapatia elimu iliyowaletea mafanikio makubwa yaliyowezesha kulima kisasa na kubadilisha maisha yao hasa katika makazi na huduma za jamii kuwapeleka watoto shule.

Aidha wakulima wamefanikiwa kununua vyombo vya usafiri vya moto kama pikipiki na kuachana na baiskeli. Hata hivyo amesema pamoja mafanikio hayo wana changamoto hasa ya masoko na elimu ambayo wanadhani wanaihitaji zaidi huku akisisitiza zaidi kwamba elimu inatakiwa hata kama wamemaliza mradi na wahisani kuondoka.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi