loader
Picha

Fainali mwigizaji mwenye kipaji Jumamosi

Shindano hilo la TMT ambalo linasimamiwa na Kampuni ya usambazaji, utengenezaji na uuzaji wa filamu ya Proin Promotions lilianzishwa rasmi Aprili mwaka huu, lengo likiwa ni kusaka na kuibua vipaji vya uigizaji kwa Watanzania wenye vipaji ambao hawakupata bahati ya kuonekana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu fainali hizo, Mratibu wa shindano hilo Joshua Moshi alisema fainali hizo zitashirikisha washiriki 10 bora ambapo atatafutwa mshindi mmoja atakayejinyakulia Sh milioni 50 na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya Proin Promotions.

“Washiriki hawa 10 waliofanikiwa kuingia katika fainali ya kuzisaka Sh milioni 50 za Kitanzania hatutawaacha hata kama hawatashinda watapewa nafasi ya kucheza filamu ya pamoja huku baadaye kuanza kunufaika na mauzo ya filamu hiyo,” alisema.

Alisema awali zoezi la kusaka vipaji hivyo liliendeshwa katika kanda tano ambazo ni kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini na kuwapata washiriki 20 ambao walikuja Dar es Salaam na kuweka kambi na hatimaye ukafanyika mchujo na kubaki 10 waliongia fainali.

MWANAMUZIKI mkongwe wa Bendi ya Kilimanjaro ‘Wana Njenje’, Mabrouk Hamis ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi