loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Fastjet kwenda Entebbe kuanzia wiki ijayo

Safari hizo zitakuwa zikifanyika Jumanne na Alhamisi na zitakuwa ni za moja kwa moja kama ilivyo kwa safari ya Dar es Salaam kwenda Harare.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Fastjet, Ed Winter alisema anaamini kuwa safari hiyo ambayo itamgharimu abiria kiasi cha dola za Marekani 50 bila kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) itasaidia kuleta ushindani kwenye sekta hiyo na itawasaidia kibiashara.

“Ninaamini kuwa safari hii mpya kati ya Tanzania na Uganda itasaidia kukuza utalii baina ya nchi hizi mbili,” alisema Winter. Aliongeza kuwa kuingia kwa Fastjet kwenye soko la Uganda inatokana na msaada walioupata kutoka Serikali ya nchi hiyo na mamlaka zake.

“Tunafurahia kuanza kwa safari hiyo Septemba 16 kwa kuwa ni mwanzo wa kujitanua kwetu nchini humo”.

Tangu Shirika la Ndege la Uganda lisitishe safari zake nchini, nauli iliyokuwa ikitozwa na ndege nyingine kwa abiria wanaokwenda na kutoka Uganda kuja Dar es Salaam ilipanda kiasi kikubwa.

Kwa sasa Fastjet inafanya safari zake za kimataifa kati ya Dar es Salaam na Johannesburg, Lusaka na Harare. Kwa safari za ndani husafari kati ya Dar es Salaam kwenda Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi