loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ferguson: Ni ujinga kumfukuza Moyes

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu pia wametolewa katika michuano ya Kombe la FA na Kombe la Ligi (Capital One), ingawa bado wako katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kiwango duni cha United kimesababisha kuwapo kwa uvumi kuwa miamba hiyo itamfukuza Moyes ikiwa ni chini ya mwaka mmoja katika mkataba wake wa miaka sita, lakini Ferguson amekataa pendekezo hilo, akisema uvumilivu ni muhimu kwa ajili ya mafanikio ya muda mrefu.

“Sielewi kwa nini klabu zinabadili makocha haraka mno,” alisema Ferguson mwenye umri wa miaka 72.

“Wao (wajumbe wa Bodi) wanapaswa kujadili ubora wa kocha wanaotarajia kumpa kazi na kwa uhakika, unapaswa kutazama wasifu wake – tabia, falsafa aliyonayo.

“Kama hivyo ndiyo walivyofanya kumpa mtu huyo kazi, kwa nini wasivumilie kuwa naye? Kwangu mimi naona ni ujinga. “Hakuna haja ya kufuata njia hiyo (kufukuza makocha).

“United inaweza kufanya chochote. Wana falsafa hiyo na historia hiyo, kila mara wanafanya vizuri.”

Wakati Ferguson alipotua Old Trafford, alikuwa ametwaa mataji 10 makubwa na Aberdeen katika Ligi Daraja la Kwanza Scotland, lakini ilimchukua misimu sita kushinda ubingwa wa ligi England.

United ilimaliza katika nafasi ya 11, ya pili, 13, sita na ya pili, kabla ya Ferguson kutwaa taji lake la kwanza la ligi na klabu hiyo katika msimu wa 1992-93.

Mataji 12 zaidi yalifuata kabla ya Ferguson kustaafu mwishoni mwa msimu uliopita – baada ya kuiongoza United kutwaa ubingwa – lakini mkurugenzi huyo wa klabu anaamini kwamwe hajawahi kuona msimu wa ligi kama wa 2013-14.

Klabu ya Liverpool na Manchester United zipo vitani kumuwinda ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi